MAHAKAMA Kuu, Divisheni ya Rushwa na Ujumumu Uchumi, Dar es Salaam imemuachia huru Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kwa kuwasilisha hati ya kutakuwa na nia ya kuendelea na mashtaka dhidi yao.
Mbowe na wenzake, Adam Kasekwa, Halfani Bwire na Mohamed Ling’wenywa waliokuwa makomandoo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wameachiwa huru leo Machi 4, 2022 na Jaji Joachim Tiganga.
Mapema kesi hiyo iliitwa mahakamani hapo kwa ajili ya washtakiwa kuanza kujitetea lakini Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando alieeleza mahakama kuwa DPP amewasilisha hati (Nolle) kuwa hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa.
Tags
habari matuko