Kundi la wawekezaji wa makampuni ya uwakala wa Utalii Wamarekani weusi
wamewasili nchi Kwa lengo la kuwekeza katika sekta ya utalii baada ya
kuvutiwa na filamu ya Royal Tour iliyofanywa na Rais Samia Suluhu
Mkurugenzi wa Natural Responsible Safari Tanzania na Uganda Kassim
Said ameeleza Kwamba ujio wa wageni hao ni fursa nzuri ya kuinua soko
la utalii.
Amesema kwamba ujio wao umewavutia wageni hao kuweza kutokana na uwepo
wa vivutio vyote katika eneo Moja ambalo halipatikani sehemu yoyote
duniani.
Akabainisha kuwa wawekezaji hao Saba watakiwa nchini Kwa siku 10 ndio
maana wamewapeleka Tanapa kupata Ili kupata taarifa za maeneo ya
vivutio vivyopo nchini.
Awali kabisa wawekezaji hao wanawasili katika makao makuu ya Shirika
la Hifadhi za Taifa la Tanzania (TANAPA) na kupatiwa taarifa juu ya
vivutio vilivyopo Tanzania na wanaeleza kilichowavutia mpaka wakafunga
safari na kuja nchini
Kwa upande wake kamishna msaidizi wa uhifadhi katika Shirika la
Hifadhi za Taifa la Tanzania (TANAPA) Beatrice Kessy amesema ujio wa
mawakala hao wa utalii kutaongeza wigo wa soko la utalii nchi ya
Marekani.
"Tumeongea nao tutakuwa tukifanya mawasilisho Kwa njia ya mkutano ya
video kuelezea vivutio vilivyopo hapa nchi kuvutia Marekani weusi kuja
nchini"
Nae Mwakilishi wa Miles Away Travel Adonica Pickeh kutoka nchini
Marekani amesema kuwa Tanzania inavyovivutio vingi kwa muda mchache
aliopata kuwepo hapa nchini ameweza kubaini hilo na wanajipanga kwenda
kujionea hifadhi ya Serengeti na baadae fukwe katika visiwa vya
Zanzibar.
"Hakuna sehemu yeyote duniani unaweza kuapata vivutio vyote katika
eneo moja la nchi kama hapa Tanzania unapata fukwe hapo hapo unapata
hifadhi za wanayamapori na kupanda mlima sanjari na malikale hii ni
sehemu muhimu na soko kubwa sana"
Marekani ni miongoni mwa mataifa yanayoongoza kwa Watalii mataifa
mengine ni pamoja na Ujerumani,Italia na Hispania huku masoko mapya
yanayokuja kwa kasi yakiwa ya nchi za Asia.
Baada ya kampeni ya kutangaza duniani raslimali za taifa kupitia
filamu ya vivutio vya utalii katika kipindi maarufu cha Royal Tour
kulikofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu
tayari wawekezaji wamenza kuvutiwa ambapo kundi la Wamarekani weusi
wamewasili nchini kwa lengo la kuwekeza katika sekta ya utalii