BREAKING NEWS

Monday, March 21, 2022

NDEGE YA SHIRIKA LA NDEGE LA CHINA YAANGUKA

 

Ndege ya shirika la ndege la China Eastern Airlines aina ya Boeing 737 iliyokuwa imebeba watu 132 imeanguka katika mkoa wa Guangxi, vyombo vya habari vya serikali ya China vinaripoti.



Idadi ya waliofariki bado haijajulikana.


Ajali hiyo, katika eneo la milimani, ilisababisha moto msituni, vyombo vya habari vya serikali vinaripoti


Ndege ya MU5735 ilipangwa kuondoka Kunming saa 13:15 na ilikuwa njiani kuelekea Guangzhou.




China imekuwa na rekodi nzuri ya usalama wa anga katika muongo mmoja uliopita.




Ajali ya mwisho kubwa ya ndege nchini humo ilikuwa Agosti 2010, wakati ndege kutoka Harbin ilipoanguka Yichun na kuua watu 42.




China Eastern bado haijatoa tamko lolote kuhusu ajali hiyo, au kujibu maswali, lakini imeondoa nembo yake kwenye akaunti yake ya Weibo na pia kubadilisha tovuti yake kwa picha nyeusi na nyeupe- ishara ya maombolezo, vyombo vya habari nchini viliripoti.




Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini China imesema kuwa wachunguzi wake wametum

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates