WATANZANIA WATAKIWA KUVAA UREMBO UNAOTAKANA NA MADINI YAO

 



Watanzania wametakiwa kutumia vitu vya madini  mbalimbali yaliopo katika nchi yetu Kwa kutengeneza na kuvaa  madini hayo Ili kuweza kutangaza  madini hayo  yanayopatikana hapa nchini
Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa Mmiliki wa kampuni ya Sendeu Agrovet Co. Ltd  Gabriel Sendeu alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ambapo alisema kuwa ni watanzania wakajijengea tabia ya kupenda vya kwao  kwani vinathama
Alisema kuwa watanzania wamekuwa hawana tabia ya kuvaa vyakwao  badala yake wanavaa vitu kutoka nje tu ambavyo vingone avina ubora na vingine 
Alisema nchi yetu Ina madini ya aina mbalimbali ambayo iwapo watanzania watajijengea tabia ya kuyavaa pamoja na kutengenezea bidhaa mbalimbali za urembo zitasaidia  kuyatangaza madini hayo
 "Tunamadini mengi sana hapa nchini ambayo watanzania tukiamua kuyatangaza Kwa kuvaa vidani vinavyotokana na madini hayo itasaidia sana kuyatangaza mfano Bora tu ni madini ya rubby yapo apa kwetu lakini Kuna baadhi ya watu hawatambui madini haya Kama yanapatikana hapa ,mengine ni madini ya Tanzanite ambayo yanapatika hapa nchinilakini kwakuwa watanzania atuna mazoea ya kuvaa vito hivyo Ili tuvitangaze watu kutoka nchi za wenzetu wanavaa na wanatumia fursa hiyo kusema yanatoka kwao"alibainisha Sendeu
Alitoa wito kwa vijana kuwekeza katika kuongezea dhamani madini kwani itawasaidia kupata kipato kikubwa ambacho kitawakwamua kimaisha
Alisema madini yana kazi mbalimbali ukitoa kazi ya kuchimba ivyo vijana wakiamua kujikita katika sekta hii itawasaidia kuweza kujiajiri na hata kuajiri watu wengine.
"uzuri wa madini haya unaweza ukaamua kujiajiri katika sekta ya kuongezea dhamani ikiwemo kutengeneza shepu za madini ,kupiga polishi kutengeneza vipuli mbalimbali pamoja na mambo mengine mbalimbali "alibainisha 
 Alisema kuwa Kwa upande wa kampuni yao imeweza kuchangia vyema pato la taifa ambapo wameshaweza kulipia tozo mbalimbali huku alibainisha kuwa wameshalipa zaidi ya milioni miatano huku mamlaka ya mapato wakiwa wamepatiwa milioni 350 
Aliongeza kuwa katika kuhakikisha wanamalizia tatizo la ajira hapa nchini wameweza kuajiri jumla ya wafanyakazi wa zawa zaidi ya 100ambao wote wanafanya kazi mgodini apo na wanapatiwa staiki zao zote 

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post