BREAKING NEWS

Tuesday, March 8, 2022

PAPU YATAKIWA KUTOA HUDUMA KIDIGITALI

 



Naibu katibu mkuu wizara ya habari ,mawasiliano na teknolojia ya habari , Mohamed Abdulah ameutaka Umoja wa Posta Afrika (PAPU) kujikita katika maboresho ya  teknolojia ya kidigitali katika kuendesha shughuli za usafirishaji wa vifurushi barani Afrika.

Akifungua Kikao cha  kamati ya fedha na Utawala (PAPU) kinachofanyika kwa siku tatu Jijini Arusha,Abdulah alisisitiza  kamati hiyo kuweka kipaumbele matumizi ya tehama katika usambazaji wa vifurushi .

Alisema pamoja na mambo mengine kikao hicho pia kitajadili masuala ya fedha na michango Kwa Nchi wanachama ili kuweza kujiendesha hasa wakati Papu inaingia kwenye matumizi ya Tehama pamoja na kukamilisha ujenzi  wa jengo la makao makuu ya PAPU unaoendelea jijini Arusha.

"Tanzania tumepiga hatua Kwa matumizi ya Tehama na hivi Sasa tuko kwenye zoezi la utambuzi wa anwani  za makazi ambapo Kwa matumizi ya shirika la posta ni hatua kubwa na tutakuwa mfano Kwa Nchi za Afrika"alisema

Naye katibu Mkuu wa PAPU ,Sifundo  Moyo alisema kuwa kipaumbele cha umoja huo ni kuhakikisha wanafikia malengo ya  kuboresha usafirishaji wa vifurushi Kwa njia ya kidigital na kila nchi wanachama itachangia njia sahihi ya uboreshaji wa shirika la posta na mamlaka ya mawasiliano .

Aidha Moya ameihalikishia serikali ya Tanzania kupitia shirika la posta kuwa litaendelea kuwapa ushirikiano wa kutosha katika kuifanya sekta ya postavkuwanya Kidigitali na yenye manufaa Kwa Jamii.

Kwa upande wake Kaimu  Mkuu wa shirika la posta Nchini,Macrice Mbodo alisema shirika la posta Nchini lipo katika hatua za maboresho ya shughuli zake ili ziendane na vionjo vya matakwa ya wateja na mabadiliko ya teknolojia duniani.

Alisema Kwa Sasa shirika hilo limefanikiwa kuunganisha usafirishaji wa vifurushi Kwa Tanzania bara na visiwani na kwamba pindi mteja atakapotuma mzigo na yule unayepokea wote watapata ujumbe wa simu yakononi ukiwafahamisha mzigo aliotumwa au kupokelewa.

"Tumeboresha shughuli zetu za posta Nchini mteja hatalazimika tena kupiga simu ofisini kuulizia mzigo aliotumwa hivi Sasa huduma za posta zipo kiganjani ,alisema

Aliongeza kuwa shirika la posta Nchini limeungana na posta zingine za nchi 192 duniani katika mawasiliano ya kusafisha vifurushi na hivi karibuni Shirika la posta litaanza kusafirisha vifurushi Kwa kutumia  Shirika la ndege ya Tanzania ATCL kwenda nchi mbalimbali ambazo ATCL inafanya safari zake.

Alisema uwepo wa miundombinu ya anwani za makazi shirika la posta limeanzisha huduma ya posta mlangoni ambayo itarahisisha kusafirisha vipeto vya mteja hadi mlangoni.

"Kwa Sasa shirika la posta tumeanzisha duka mtandao ambalo  lina bidhaa nyingi ambapo mteja atalazimika kuagiza chochote atakacho ,Kwa kutumia anwani za makazi  utaletewa hadi mlangoni ."alisema

Naye mwenyekiti wa kamati ya fedha na Utawala PAPU akiwakilishaTanzania katika kikao hicho, Abdulah Migila  ,alisema kamati hiyo itajadili Kwa siku tatu namna ya kupata fedha kupitia michango ya Nchi wanachama na masuala ya Rasilimali watu.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates