Watatu kushoto afisa ushirika mkoa wa Arusha mkubwa Musa akimkabidhi baadhi ya zawadi zilizotolewa na wanawake wa chama Cha Arusha women business saccos LTD ,daktari kutoka kitengo cha magonjwa ya Kansa katika hospital ya rufaa ya Kanda ya kaskazini (KCMC) Dr.Atukuzwe Kahakwa kwaajili ya wagonjwa wenye ugonjwa wa saratani mbalimbali waliopo katika hospital ya rufaa ya Kanda ya kaskazini (KCMC)ambapo mbali na kukabidhi vifaa hivyo waliwachangia pia damu zaoezi lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hotel ya Coridr spring iliopo ndani ya halmashauri ya Jiji la Arusha (Woinde Shizza)
Na Woinde Shizza , ARUSHA Watanzania wametakiwa kujijengea tabia ya kuchangia damu mara Kwa mara Ili kuweza kupunguza tatizo hilo la upungufu wa damu salama katika benki ya damu pamoja na kuwasaidia watoto pamoja na watu wazima wenye tatizo la saratani (Kansa)za aina mbalimbali Hayo yamebainishwa na daktari kutoka kitengo cha magonjwa ya Kansa katika hospital ya rufaa ya Kanda ya kaskazini (KCMC) Dr.Atukuzwe Kahakwa alipokuwa akiongea katika sherehe za maadhimisho ya wiki ya wanawake duniani yaliandaliwa na kikundi cha Arusha women in business saccos ltd yaliyofanyika katika ukumbi wa Arusha corridor spring ambapo maathimisho hayo yalitanguliwa na maandamano ya wanawake hao Alisema kuwa katika kitengo saratani kunauhitaji mkubwa sana wa damu kutokana na wagonjwa wengi wa Kansa kutakiwa damu nyingi ,kwani baadhi yao ugonjwa huo unasababisha kupunguza damu Kwa kasi kubwa "Mfano pale kwetu KCMC katika kitengo Cha Saratani tumekuwa tunapokea watoto wengi wenye ugonjwa wasaratani ya damu hivyo unakuta kutokana na tatizo hilo damu yao inaisha mapema na ikisha Isha tunashidwa kumpa mgonjwa huduma adi pale anapoongezewa damu pia mfano Saratani ya damu inatabia ya kushusha damu sana hivyo tunawaomba watanzania wenzetu wawe wepesi kujitokeza kuchangia damu kwani Kila mmoja akichangia damu anaenda kuokoa maisha ya watu fulani pia damu ni uhai na ukombozi ,pia labda niwashukuru Benki ya damu Tanzania wamekua wakijitaidi sana kukusanya damu Kwa ajili ya wagonjwa alisema Atukuzwe Alisema saratani wanazozipokea kwa wingi kwa upande wa watoto saratani ya damu ndio inawakumba sana watoto ,Kwa wanawake saratani ya matiti na Kwa wanaumw saratani ya tezi dume ndio inawakumba sana wababa. Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya chama cha Arusha women business saccos ltd Lusinde Urasa alisema kuwa katika kusherekea siku hii ya wanawake duniani katika chama chao wameona warudishe fashila zao Kwa wagonjwa wa saratani mbalimbali waliopo katika hospital ya KCMC ambapo wameamua kuchangia damu wagonjwa wao pamoja na kuwapatia viti mbalimbali ambavyo walikuwa wakiviitaji Alisema tatizo hilo linaonyesha ni kubwa hivyo ni vyema watanzania wakajitoa zaidi katika swala hili Ili kuweza kuokoa maisha ya watanzania wenzao ambao wanasumbuliwa na magonjwa mbalimbali ambapo pia wanahuitaji wa damu Nae mgeni rasmi wa maathimisho hayo afisa ushirika mkoa wa Arusha mkubwa Musa aliwapongeza wanawake wa chama hicho na kuwaambia waendelee kuwa na moyo huo huo wakujitoa Kwa wenyeuhitaji huku akiwasihii kuendelea kuwa waaminifu na wawe wanarejesha vyema fedha ambazo wanachukuwa katika chama chao Ili kuondoa tatizo hilo kwani wanavyorejesha vyema fedha hizo atapewa mwanamke mwingine na zitaenda kumuinua na atapewa maarifa yatakayo msaidia kiendeleza maisha Aidha pia aliwataka wanawake kutengeneze mipango bila ya kuwa na mipango hawataweza kufikia malengo yao Kama walivyokusudia. Kwa upande wake meneja wa chama hicho Maria Mange alisema kuwa chama chao kimepata mafanikio ma kubwa tangu kuanzashwa kwani Kwa sasa wanawanachana 900 wakati walipoanzisha walianza na wanachama 20 ,ambapo pia alisema hadi walishakopeshana zaidi ya shilingi bilioni 20 Alitaja kaulimbiu ya maathimisho haya Kwa mwaka huu inasema kuwa kizazi cha haki na usawa kwa maendeleo endelevu.
|
Tags
habari matuko