BREAKING NEWS

Tuesday, March 15, 2022

KAMATI YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMIIIMETEMBELEA TAASISI YA NELSON MANDELA



Na Mwanaidi Bundala


 Kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii imetembelea taasisi ya Afrika ya Sayansi na Technologia ya Nelson Mandela NM -AIST imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya kituo atamizi na kiwanda darasa, pamoja na mradi wa ujenzi wa hosteli 


Akitoa taarifa ya miradi hiyo Makamu mkuu wa Chuo kikuu cha Nelson Mandela Prof. Emanue Luoga alisema kuwa, Chuo hicho, kinahusika na maswala ya technologia na ubunifu katika bajeti ya mwaka 2020-2022 ambapo inapata ruzuku kutoka serikali bilioni 1 na milioni 44, na mapato ya ndani fedha ya za utafiti kutoka kwenye miradi ya ndani ya Chuo .


Alisema kuwa Katika kipindi cha mwaka 2021/22 taasisi ilitengewa kiasi cha shilingi 19,733,597,932 ambapo kati ya hizo shilingi 7, 96, 766,000 ni mishahara ya wafanyakazi na shililingi 280, 880,108 ni matumizi mengineyo shilingi 6,55,000,000 kwa ajili ya utafiti wa ubunifu kutoka kwa wadau wa maendeleo na shilingi 1,044,053,820 kutoka serikalini kwa ajili ya miradi ya maendeleo.


Alisema kuwa, kutekekeza miradi wa bilioni 1.5 kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa mabweni ya wanafunzi na milion 344a kutekekeza miradi wa bilioni 1.5 kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa mabweni ya wanafunzi 500


Alisema kuwa wanajenga mabweni ambayo yatakuwa pacha matatu ambapo majengo 2 yatakuwa na uwezo wa kubeba wanafunzi 180 kila moja na jengo la Tatu litakuwawna uwezo wa kubeba wanafunzi 140 na ma bweni hayo yatatoa kipaumbele kwa wanafunzi wa kike wanaolea .

 

Kwa upande wake waziri wa Elimu Sayansi na Technologia Mh.Adolf Mkenda Alisema kuwa, miradi hiyo ni muhimu Sana katika kuendeleza Chuo hicho na kuongeza zaidi wanafunzi kutoka nje ya nchi.


Nae mwenyekiti Baraza la chuo Prof. Joseph Mbushweshija alisema kuwa Chuo kinatakiwa kupata wanafunzi wengi kutoka nje ya nchi ili kuweza kuwaenzi waanzilishi wa Chuo hicho ili kiweza kupata maendeleo kupitia Sayansi na Technologia 


Alisema kuwa Chuo hicho kitafika mbali na aliwataka waheshimiwa wabunge kukisemea Chuo hicho bungeni ili kuweza kuongeza bajeti na pia baraza la Mikopo kutoa fungu ili wanafunzi waweze kuja kusoma na kuwa mhimili mzuri wa kukuza Sayansi na Technologia 



Alisema kuwa, Chuo hicho pia kimekuwa ni 

Washiriki wakubwa sana wa mashindano ya Makisato , nanenane, na vyuo vikuuu ili wanafunzi kuweza kuonyesha technologia walizonazo ikiwa ni pamoja na kushiriki maonyesho na ubunifu unaolenga kutatua changamoto katika jamii na viwanda 


Alisema mikakati kusambaza maswala ya technologia na ubunifu katika bajeti ya mwaka 2022 ruzuku kutoka serikali bilioni 1 na milioni 44, na mapato ya ndani fedha ya utafiti kutoka kwenye maswala ya utafiti 


Katika kutekekeza miradi wa bilioni 1.5 kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa mabweni ya wanafunzi na milion 344


Mradi wa ujenzi wa Bweni litachukua wabafunzi 500 ambalo litakuwa na vyumba maalumu hada kwa kinamama wenye mahitaji maalumu ya kulea ili kuweza kuwapa nafasi ya kuendelea na malezi na shughuli za masomo 


Alisema kuwa mradi huu unasimamiwa na Chuo cha Ufundi Arusha ambapo ulianza October mwaka jana ambapo wanatarajia kumaliza ujenzi huo mwezi wa tatu 2023




Pia alieleza changamoto za ufinyu wa Bajeti, upungufu wa miundombinu, uhaba wa watumishi hasa wanataaluma ikiwemo uhaba wa watumishi hasa wa Taaluma ya maprofesa, wahadhiri waandamizi 40, wahadhiri 13, na wahadhiri wasaidizi 14, na watumishi mwega 12.


Kwa upande wao kituo Atamizi na kiwanda darasa akiwemo Profesa Evodius Rulaz ambaye ni mtaalamu Wa kukausha mazao mbalimbali ya kilimo, Dr. John Nyika, na Profesa Geofrey Raymond ambaye ni Mwana Sayansi wa Afya aliweza kutengeneza dawa dawa mbalimbali za binadamu ambazo zitaanza kuingia sokoni na kusaidia jamii Kutibu magonjwa mbalimbali.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates