Na Teddy Kilanga, Arusha.
Kutokana na tatizo la baadhi ya vijana kutokuwa uadilifuwanapopata nafasi ya uongozi Katibu tawala wa mkoa wa Arusha,Dkt.Athuman Kihamia amewataka vijana kuwa na weledi na uzalendo katika kulitumikia Taifa lao
Dkt.Kihamia amesema hayo katika hafla ya kukabidhi vyeti kwa wanafunzi wa kozi fupi ya uanagenzi yaliyodhaminiwa na Ofisi ya waziri mkuu,kazi vijana,ajira na watu wenye ulemavu,katika chuo cha Taifa cha Utalii ambapo ameeleza kuwa sasa hivi Taifa linakabiliwa changamoto ya utovu wa maadili kwa vijana.
Aidha Kihamia amesema tatizo hilo linawahangaisha wao kama serikali katika kubuni mbinu mpya ya kutafuta kukabiliana na changamoto hiyo lakini inakuwa ngumu hivyo amewaomba vijana waliyohitibu chuo cha Taifa cha utalii Arusha wawe wazalendo wa Taifa lao.
"Wawe wazalendo wa nchi yao katika kuwa waadilifu,waaminifu na wazalendo katika nchi yao kwani jambo hili litasaidia serikali kurahisisha kufanya mipango yake ya kutekelezeka kwa urahisi zaidi,"amesema Kihamia.
Kihamia amesema sasa hivi unaweza kuajili vijana kadhaa baada ya muda mfupi waweza sikia wameiba wengine kutoa lugha ya matusi kwa mabosi wao hali hiyo huleta taswira mbaya kwa vijana hivyo tunajitahidi kama serikali ili kizazi cha sasa kiweze kubadilika.
"Lakini naamini mafunzo mliyopata hapa yatakwenda kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii na mambo yasiyo ya lazima kuhakikisha hayatatokea,"amesema Dkt.Kihamia.
Amesema mafunzo hayo waliopata yatakuwa chachu katika kuongeza ubunifu na kuwajenga vijana katika ujuzi utakaowasaidia kuongeza wigo mpana wa kuajiriwa.
Naye Meneja wa chuo cha Taifa cha utalii Arusha,Dkt Maswet Masinda amesema kati ya wanafunzi 111waliyohitimu mafunzo hayo 17 wameshaajiriwa katika sehemu mbalimbali mkoani Arusha.
Hivyo tunachoomba wanafunzi hawa wazingatie mafunzo waliyoyapata na kuyatumia vyema katika sehemu zao za ajira,"amesema.
Aidha amesema wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa eneo la ujenzi wa bweni la wasichana huku mikakati yao mingine ni kujenga madarasa ya kisasa na jengo la utawala pamoja na kuongeza udahili wa wanafunzi.
Baadhi ya wanafunzi waliohitimu wameishukuru serikali kwa kuwadhamini masomo hayo kwani sasa hivi wamepata sifa za kuajiriwa sehemu yoyote hivyo wamehaidi kufanya kazi kwa weledi