BREAKING NEWS

Tuesday, March 22, 2022

SERIKALI YATAKIWA KUWEKEZA KATIKA ZAO LA PARACHICHI ILI KUPUNGUZA TATIZO LA UHABA WA MAFUTA YA KUPIKIA

 


Na Woinde Shizza,Arusha

 

Serikali imeobwa kuwekeza nguvu katika kilimo cha la parachichi kwani soko la zao hilo ni kubwa ndani ya nchi na nje ya nchi pia litasaidia kupunguza tatizo la uhaba wa mafuta unaopelekea bei kupanda.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya AVOMERU GROUP  inayojihusisha na mafunzo na ubunifu ya kuchataka bidhaa za maparachichi  Jesse Oljange alipokuwa akiongea na waandishi wa habari walipokuwa katika ziara ya mafunzo ya kuandika habari za sayansi na teknnolojia yalioandaliwa na Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu (COSTECH) yaliyofanyika kwa muda wa siku tatu katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Arusha na kufuatiwa na ziara ya siku mbili ya kutembelea taasisi zinazojishulisha na kazi za sayansi na teknolojia

Alibainisha kuwa  tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta nchini limekuwa kubwa kwani kila siku bei ya mafuta imekuwa ikipanda zaidi hivyo katika kuangalia namna ya kupunguza tatizo hilo kama sio kuondoa kabisa ni vyema    Serikali  kuamua  kuwekeza kwenye viwanda  vidogo vinavyozalisha mafuta ya parachichi ili kufanya mafuta hayo kutumika kwaajili ya chakula

 

“mbali  ya chakula pia zao hili la parachichi linaitajika kwa kiasi kikubwa  nje ya nchi kwani mbali na kutumika kwa ajili ya chakula pia zao hili mafuta yake yanatujika kwa matumizi mbalimbali kama kutengenezea mafuta ya nywele,mafuta ya ngozi na pia tunda lake hutumik a kwa ajili ya kutengenezea vyakula mbalimbali”alisema Jesse

 


Alieleza kuwa zao hilo linafursa nyingi ikiwemo kutunza mazingira, ni tunda, pia mbali na kukamuliwa mafuta pia kokwa lake kutengenezewa bidhaa za kutunza ngozi hivyo ifike mahali wakulima wawekeze katika zao hilo ka wingi kwani linachangia katika ukuaji wa uchumi.


Aidha alisema kuwa  uwepo wa kampuni hiyo tangu kuanzishwa umesaidia  wakulima wa zao hilo la parachichi kuongeza vipato vyao  na kuweza kuendesha maisha yao na sio mkulima tu bali imesaidia kukuzapato la taifa na kuingizia fedha za kigeni pale wanapoenda kuuza mafuta hayo nje ya nchi

 

baadhi ya waandishi wa habari wakifatilia maelezo kutoka kwa
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya AVOMERU GROUP  inayojihusisha na mafunzo na ubunifu ya kuchataka bidhaa za maparachichi  Jesse Oljange  walipotembelea ofisini kwake

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates