BREAKING NEWS

Thursday, March 17, 2022

TATIZO LA KUWEPO KWA FLORIDE KWENYE MAJI MBIONI KUMALIZIKA


waandishi wa habari pamoja na watafiti wakiwa katika picha pamoja wakati  mafunzo ya siku tatu ya waandishi wa habari na watafiti wa Kanda ya Kaskazini yaliyoandaliwa na Tume ya taifa ya sayansi na teknolojia (COSTECH) yanayofanyika mkoani Arusha 


waandishi wa habari wakifatilia mada wakati wa mafunzo ya siku tatu ya waandishi wa habari na watafiti wa Kanda ya Kaskazini yaliyoandaliwa na Tume ya taifa ya sayansi na teknolojia (COSTECH) yanayofanyika mkoani Arusha 


 Na Woinde Shizza , ARUSHA 


Tatizo la madini ya Floride na Chumvi kwenye maji linaloikabili baadhi ya mikoa nchini huenda likapatiwa ufumbuzi baada ya mtafiti mzawa Salvatory Rubangira kugundua dawa za kusafisha maji zilizopewa majina ya TANBEZI na TANCIDI.


Mtafiti kutoka taasisi ya utafiti ya Milemine East retaining (MERCO) alianza kufanya tafiti zake mwaka 1983 Kwa kutembelea zaidi ya mapori zaidi ya 73 ya Tanzania na nchi jirani na kugundua dawa mbalimbali zitokanazo na mimea.


Akiongea na waandishi wa habari katika mafunzo ya siku tatu ya waandishi wa habari na watafiti wa Kanda ya Kaskazini yaliyoandaliwa na Tume ya taifa ya sayansi na teknolojia (COSTECH) yanayofanyika mkoani Arusha alisema kuwa aliamua kutengeneza dawa hizokutokana na kuona tatizo hilo kuzidi kuongezeka katika mikoa ya Arusha , Kilimanjaro na Manyara.


Alisema dawa hizo zinauwezo wa kusafisha maji na kuondoa Floride kwa asilimia 85 na Kuna baadhi ya watu wameshaanza kutumia dawa hizo na kupata matokeo mazuri.


"Maji haya yenye Floride yanatajwa kuwa na athari kubwa Kwa binadamu na inaathiri watu wengi mfano tosha ni watu wa Kanda hii ya kaskazini wengi wao ukiwaangalia ata meno yamebadili rangi na hata pia yanaathiri mifupa haswa haswa Kwa upande wa mifupa linawaathiri zaidi watoto wengi wao unawakuta wanaipata matege "alisema


Alibainisha kuwa Kwa sasa anazalisha kwa kiasi kidogo kulingana na kutokuwa na vitendea kazi vya kuzalisha Kwa wingi kulingana na mahitaji hivyo aliomba serikali kumueezesha aweze kuzalisha Kwa wingi.


Alisema kuwa mbali na kufanya utafiti wa dawa hizo za kusafisha maji pia ameweza kufanya utafiti wa dawa mbalimbali ikiwemo dawa za kutibu magonjwa ya wanawake ,dawa za kutibu magonjwa ya ngozi ,dawa za kutibu magonjwa ya macho pamoja na dawa ya ugonjwa wa uzio.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates