BREAKING NEWS

Tuesday, February 22, 2022

TANESCO ARUSHA YAANZA PROGRAM YA KUMALIZA MALIPO YA 27000

Meneja wa shirika la umeme TANESCO mkoa wa Arusha  Herini Muhina akiongea na Wananchi wa kata ya Terati wilayani Arusha   mkoani Arusha  katika ziara iliyofanyika kwenye Kata hiyo ambapo alisema  hadi kufikia mwezi Desemba mwaka jana jumla ya wateja 73 walifanya malipo yao ambapo amesema zoezi la kuwaunganishia umeme litakamilika ndani ya wiki hii

Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini Mrisho Gambo akiongea na Wananchi wa kata ya Murieti iliopo ndani ya halmashauri ya Jiji la Arusha mkoani Arusha alipokuwa katika mkutano wa adhara uliolenga kusikiliza matatizo mbalimbali ya Wananchi



 Na Woinde  Shizza , ARUSHA


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)Mkoa wa Arusha limeanza programu mahususi ya kumaliza malipo ya shilingi elfu ishirini na saba ambayo yalifanyika baada ya bei mpya kutangazwa katika Kata ya Terati na Muriet Mkoani humo.

Akizungumza na wananchi katika ziara iliyofanyika kwenye Kata hizo mbili,Meneja wa TANESCO Mkoa wa Arusha Herini Mhina amesema katika Kata ya Muriet hadi kufikia mwezi Desemba mwaka jana jumla ya wateja 73 walifanya malipo yao ambapo amesema zoezi la kuwaunganishia umeme litakamilika ndani ya wiki hii.

Aidha amesema katika Kata ya Terati jumla ya wateja waliofanya malipo ni 53 nao wataunganishiwa umeme ndani ya wiki hii ikiwa ni sambamba na pending za survie ambazo zitafanyika zote na wananchi kupata control namba .

Ameongeza kuwa programu hiyo iliuozinduliwa itaenda kimkoa ambapo baada ya kukamilika kwa Kata hizo wataelekea katika maeneo yenye wateja wengi ikiwemo Wilaya ya Arumeru lengo likiwa ni kuhakikisha mteja anafungiwa umeme ndani ya siku 7 baada ya kufanya malipo.

Vilevile Mhina ameeleza kuwa mikakati ya shirika ndani ya mwaka huu ni kuweka mfumo wa ujazaji fomu katika mtandaoni ili kumpunguzia mteja adha ya kwenda katika ofisi za TANESCO kila mara na kuokoa muda.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mrisho Gambo katika ziara hiyo amelipongeza shirika hilo kupitia Waziri wa Nishati Januari Makamba na menejimenti yote kwa kasi waliyoianza kuionyesha katika jimbo la Arusha mjini kwa ajili ya kushughulika na matatizo ya wananchi.

Mbunge huyo amewataka wananchi wa jimbo hilo hususani wale  walio katika Kata ambazo programu hiyo itatekelezwa kuhakikisha wanafanya matayarisho yote mahususi ikiwa ni pamoja na kutandaza nyaya katika nyumba zao kwa mujibu wa taratibu zote sambamba na kufanya malipo ya elfu ishirini na saba ili waweze kupata huduma hiyo ya umeme.


"Kuna kazi mbili,kazi ya serikali kutimiza wajibu wake lakini kuna kazi pia wewe mwananchi mwenyewe kutimiza wajibu wako ili kazi ya serikali iweze kuwa kazi rahisi zaidi."alisisitiza Mbunge huyo

Ameeleza kuwa hatua ya TANESCO kuanza kutandaza nguzo katika eneo la Olepolosi Kata ya Terati ni hatua nzuri naya kupongezwa kwani tangu nchi ipate uhuru eneo hilo lilikuwa na umeme mkubwa ambapo umeme mdogo haukuwahi kuwepo kwa wananchi hivyo ahadi zilizotolewa za kutekeleza mipango yao ni ahadi nzuri na inapaswa kupongezwa.

"Tanesco wametuahidi kwamba ndani ya wiki hii kabla ya ijumaa nguzo zitafika hapa na mchakato wa kuzisimika utaanza na wananchi wataanza kupata umeme hilo kwetu sisi ni jambo kubwa sana na tunawapongeza sana kwa kazi hiyo kubwa na nzuri."alisemaGambo

Awali wakiwasilisha matatizo  yao baadhi ya wananchi wa kijiji cha Nadosoito Kata ya Muriet wameiomba Tanesco kutotumia siasa katika utoaji wa huduma za umeme kwa wananchi kwani imekuwa ni kero kubwa kwa wananchi kukaa muda mrefu bila kuunganishiwa umeme baada ya kufanya malipo.

Vilevile wameomba kuangaliwa kwa maeneo mazuri kwa ajili ya kusimika nguzo za umeme na kuzitoa katika mashamba ya watu sambamba na kusimika nguzo katika mashimo ambayo tayari walishayachimba na kukaa wazi kwa muda mrefu sasa.

Akijibu matatizo  hayo Mhina amesema kuwa wananchi wote waliolipa malipo ya shilingi elfu ishirini na saba wanaenda kuunganishiwa umeme ndani ya wiki hii  ambapo pia wanamipango mbalimbali ya kuwahudumia wananchi kipitia mradi wa ujazilizi 2B kipitia REA. 

Hata hivyo wananchi wa Kata hizo mbili pamoja na tatizo la umeme linayowakabilia ambapo tayari imepatiwa ufumbuzi kupitia mradi wa Ujazilizi pia wanakabiliwa na tatizo la maji na miundombinu mibovu ya barabara ambayo imekuwa ikikwamisha kuendelea kwa shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates