Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameipongeza Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kwa kazi kubwa waliyoifanya kuwaletea maendeleo wanawake na kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na kuandaa mdahalo wa wanawake na Muungano.
Pia, ameupongeza umoja huo kwa kuendelea kuwa kinara katika kubuni na kutengeneza mambo mbalimbali yenye lengo la kuimarisha CCM, kikiunganisha na wananchi na kuimarisha umoja na mshikamano na wananchi.
Dkt. Mwinyi amesema hayo jijini Dar es Salaam leo Aprili 25, 2024 alipofungua mdahalo wa kitaifa wa Wanawake na Muungano uliondaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na kufanyika katika ukumbi wa Mlimani City.
Mdahalo huo uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wake za viongozi wakuu wastaafu, mawaziri, naibu mawaziri, wabunge, wawakilishi, wananchi na wanachama wa jumuiya hiyo na wa CCM.
Kwa upande wake mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg. Mary Pius Chatanda amesema
Taifa Mary Chatanda, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Wanawake na Muungano kuadhimisha Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam leo 25-4-2024.(Picha na Ikulu)