Mwenyekiti wa bodi ya wakala wa usalama na afya mahala pa kazi atembelea banda la kiwanda cha A to Z

 






Mwenyekiti wa bodi ya wakala wa usalama na afya mahala pa kazi Adelhelm James Meru amefurahishwa na kona uwekezaji mkubwa uliowekwa katika vifaa vya kazi mahala pa kazi kutoka kiwanda cha A- Z baada ya kujionea vifaa mbali mbali vinavyo saidia watumishi katika kutekeleza kazi zao kwa urahisi na pia kujikinga na ajali mbali mbali wanapo kuwa katika majukumu yao ya kila siku viwandani .




Aidha Mwenyekiti ameyasema hayo baada ya kutembelea maonyesho ya mabanda katika viwanja vya General tyre Jijini Arusha kwa lengo la kukagua mabanda pamoja na kujionea majukumu ya utekelezaji wa vifaa vinavyo tumika mahala pa kazi .




Akitoa ufafanuzi kwa Mwenyekiti wa bodi ya Osha nchini Injinia Harryson Rwehumbiza amesema kuwa kuna tija kubwa katika kuendelea kuwa na maonyesho hayo kwani yanakutanisha taasisi mbali mbali kujali na kuboresha vifaa vya watumishi mahala pa kazi ambapo ameeleza kwamba pasipo na usalama kwa mtumishi katika eneo la kazi ni vigumu kupata uzalishaji bora wenye soko la ushindani kwa bidhaa zetu na zile zinazo zalishwa nje ya nchi 



Hata hivyo Kilele cha maadhimisho ya kimataifa ya usalama na afya mahala pa kazi yatafunguliwa na Naibu waziri Mkuu,na waziri wa nishati Dotto Biteko .




Kauli mbiu kwa mwaka huu ni Athari za mabadiliko ya tabia ya nchi katika usalama na afya kazini Sajili eneo la kazi Osha katika harakati za kupunguza athari hizo .


Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post