Ticker

6/recent/ticker-posts

UPO UMUHIMU WA KUTAMBUA USALAMA WA MTANDAO ILI KUJILINDA DHIDI YA UDHALILISHAJI

Imebainika kuwa upo umuhimu wa kutambua usalama wa mtandaoni ili kujilinda dhidi ya udhalilishaji au upotevu wa taarifa ambazo ni siri.



Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Taasisi Zaina foundation Zaituni Njovu wakati akitoa mafunzo ya siku mbili kwa wanawake  waandishi wa habari na pamoja na wanawake kutoka taasisi mbalimbali za kiraia   ya namna ya kuzuia matatizo ya  mtandao

Alisema njia moja wapo  ya usalama mitandaoni ni kuepuka kuweka wazi kila taarifa ambayo ni muhimu ikiwemo umri hali ya afya na mambo ya kifamilia.


 



“Ni vyema kutumia mitandao kwa kufuata kanuni na tahadhari ili kuwa salama na kuepukana na (cyber-crime) uhalifu wa mtandaoni” alisema Zaituni.


Amesema elimu hiyo ni muhimu kwa jamii ili kuongeza ujuzi na maarifa kwa watumiai na kubaini viashiria vya uhalifu mapema.



Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo wameahidi kuyafanyia kazi na kuwa mabalozi kwa wengine lengo ni kuhakikisha jamii ipo salama katika matumizi ya mitandao ambayo kutokana na dunia ilivyo hayaepukiki.

Post a Comment

0 Comments