SERIKALI YA RAIS SAMIA YATOA YATOA ZAIDI YA BILIONI MBILI YA KUFANIKISHA MIRADI YA MAENDELEO SIMANJIRO

 Na Mwandishi wetu, Simanjiro


DIWANI wa Kata ya Loiborsiret Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Ezekiel Lesenga Maridadi amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya shilingi bilioni 2 na kufanikisha miradi ya maendeleo kwenye eneo hilo.

Lesenga ameyasema hayo kwenye mkutano wa wakazi wa Kijiji cha Loiborsiret wa kueleza na kusoma utekelezaji wa ilani ya CCM na kueleza mafanikio ya miaka mitatu ya Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan na kusikiliza kero na changamoto za jamii ya eneo hilo.

Diwani huyo amesema Rais Samia amefanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye kata yake ya Loiborsiret hivyo ni jukumu la jamii ya eneo hilo kumuunga mkono pindi ukifika muda wa uchaguzi mwaka 2025.

"Rais Samia hoyee tunamshukuru kwa kutumwagia miradi mingi ya maendeleo kwenye kata yetu ya Loiborsiret na tunamuahidi kuwa naye kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka kesho kwa kumpa kura zote za ndiyo," amesema Lesenga.

Amesema hadi hivi sasa kwenye vijiji vyote vitatu vya kata ya Loiborsiret vya Kimotorok, Narakauo na Loiborsoit, vimepata umeme na daraja la Loiborsiret limejengwa.

"Kituo cha afya kata ya Loiborsiret ujenzi unaendelea, jengo la mama na mtoto tayari, ukarabati wa bwawa la Narakauo limekamilika na maji yapo ya kutosha," amesema Maridadi.

Diwani huyo amesema barabara ya kutoka Korongoni kwenda Loiborsiret hadi kitongoji cha Irmang'wa kwa sasa inapitika kwa nyakati zote.

"Uanzishwaji wa shule shikizi katika maeneo ya kata ikiwemo shule shikizi iliyokamilika ya Oltepeleki kijiji cha Loiborsiret, shule shikizi ya Noomoton kijiji cha Narakauo," amesema Maridadi.

Amesema pia umefanyika ujenzi wa shule shikizi mtoni kijiji cha Narakauo, shule shikizi Noomokon kijiji cha Narakauo na shule shikizi ya Olmoti iliyopo Kijiji cha Loiborsiret," amesema.

Amesema pia umefanyika ujenzi wa madarasa mapya matatu yaliokamikika katika shule ya msingi Loiborsiret, ukamilishaji wa madarasa matatu shule ya msingi Kangala na ujenzi wa maabara shule ya sekondari Loiborsiret.

"Pia ujenzi wa computer lab shule ya sekondari Loiborsiret na ununuzi wa computer kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Loiborsiret," amesema Diwani huyo.

Amesema hivi sasa kuna ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Kimotorok ambao bado unaendelea.

Mmoja kati ya wakazi wa kijiji cha Loiborsiret, Kalai Mollel amesema wameona jitihada za Diwani wao katika kuwasomea ili wapate maendeleo hivyo anapaswa kuungwa mkono.

Mkazi mwingine Leronjo Lembaji amesema hadi hivi sasa wakazi wa eneo hilo wameona jitihada kubwa zilizofanywa na Diwani wao.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post