Baadhi ya wakina Mama wanaojihusisha na uchekechaji wa mchanga wa madini ya Tanzanite mji wa Mererani
Wachimbaji Wadogo Madini ya Tanzanite mji wa Mererani wamewatupia lawama wanasiasa kukuza migogoro ya wachimbaji wadogo na wakubwa Kwa kutokemea uovu wakihofia kukosa nafasi katika chaguzi zinazofuata.
Wanasiasa hao hawajawajibika ipasavyo Kudhibiti migogoro hiyo wakihofia siasa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 utakaohusisha wabunge na madiwani.
Wakizungumza Kwa nyakati tofauti na chombo hiki baadhi ya wakazi wa Mererani wamesema kuwa Mgogoro wa kuchukuliwa na kuzuiwa Kwa njia za Wachimbaji Wadogo na wachimbaji wakubwa unasababishwa na wanasiasa kuogopa kusema Ukweli wakihofia kukosa nafasi za kugombea uongozi wa kuchaguliwa.
Mkazi wa Mererani Bi Zaituni Saidi Fundikira alisema inashangazwa kwa sasa zaidi ya vijana 1000 kukosa ajira lakini wanasiasa hawaoni kama kuna shida.
"Migodi ya wachimbaji wadogo zaidi ya mitano imefungwa na mchimbaji mkubwa Fronone ambaye anamahusiano na wanasiasa Sasa imekuwa adha Kubwa katika mji wetu wa Mererani "alisema Zaituni
Mkazi mwingine wa Mererani Kanaeli Minja alisema hivi karibuni Waziri wa madini Anthony Mavunde alipotembelea Mererani hakupewa nafasi na wanasiasa kusikiliza kero za wananchi wa Mererani badala yake alikabidhi tuzo kwa wamiliki wa migodi wanaosaidia Jamii bila kusikiliza kero zao.
Alisema walitegemea Waziri Mavunde angetoa tamko kuhusu migogoro ya Mererani lakini badala yake akawataka wachimbaji wenyewe wakae na kumaliza migogoro yao.
"Waziri alipaswa kujua kwa kuzuiliwa njia za Wachimbaji wadogo kunapelekea hali ngumu ya maisha na kuuwa mji wa Mererani ambapo watu wengi waliojiajiri wamekosa fursa ya kufanya Biashara"alisrma
Kumekuwepo na Mgogoro wa muda mrefu kati ya wachimbaji wadogo na mchimbaji mkubwa ambaye analalamikiwa kuingilia njia za mkondo wa madini wa wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite na hivyo kusababisha migogoro ya mara Kwa Mara.