Jumla ya wasichana 217453 wenye kuanzia miaka 9 hadi 14 kutoka Wilaya za mkoa wa Tanga,wamelengwa kuchanjwa chanjo ya kinga dhidi ya virusi vinavyosababisha saratani za aina mbalimbali ikiwamo ya mlango wa kizazi ikiwa ni jitihada za kuzuia ongezeko la maradhi hayo kwa wanawakw Tanzania .
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Batilda Buriani ametoa taarifa hiyo leo wakati akielezea shughuli zitakazofanyika wakati wa maadhimisho ya wiki ya chanjo Afrika itakayofanyika kuanzia jumatatu hadi jumamosi ijayo.
Amesema katika wiki hii Serikali imelenga kuimarisha zaidi utoaji wa chanjo dhidi y saratani ya mlango wa kizazi (HPV) kwa wasichana wa umri wa miaka tisa hadi 14 ambapo idadi ya waliolengwa ni 227,453 watafuatwa maeneo mbalimbali zikiwamo shule na nyumbani.
"Nchini Tanzania chanjo hii iliidhinishwa na Shirika la Afya Duniani na Wizara ya Afya kupitia Mamlaka ya Dawa na vifaa tuba (TMDA) mwaka 2014 ambapo ilianza kutumika rasmi mwaka 2014 Mkoani Kilimanjaro na mwaka 2018 nchi nzima"amesema Balozi Batilda.
Amesema hata hivyo utoaji wa chanjo hiyo ya HPV utakuwa ni dozi moja badala ya mbili zilizokuwa zikitolewa awali kutokana na tafiti za kisayansi kubainisha inatosha kutoa kinga kamili dhidi ya maambukizi ya saratani ya mlango wa kizazi.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema chanjo hiyo ya HPV kwa umri wa miaka tisa hadi 14 itafikia tamati disemba mwaka huu na kwamba mwaka januari 2025 walengwa watakuwa ni wasichana wa umri wa miaka tisa pekee.
Mariam Hassan (56) wa Ngamiani Jijini amesema chanjo hiyo itakuwa mkombozi kwa wanawake kutokana na kukngezeka kwa wimbi la saratani ya mlango wa kizazi inayosababisha vifo kila siku.
"Uamuzi wa kutoa chanjo hii kwa mabinti zetu ni wa kuungwa mkono kwa sababu wimbi la kansa ya mlango wa kizazi inatishia sana uhai wetu wanawake...itaweza kusaidia kizazi kijacho kunusurika"amesema Mariamu.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia