CHADEMA WACHACHAMAA WAKISEMA MPAKA KIELEWEKE
MGOMBEA wa kiti cha Ubunge jimbo la Arusha mjini,Godbless Lema amemtupia lawama mgombea mwenzake wa chama cha mapinduzi CCM,Batilda Burian kuwa ndiye chanzo cha kuhamishwa ghafla kwa mkurugenzi wa jiji la Arusha.
Lema alibainisha hayo mwishoni mwa wiki mara baada ya kutambulishwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea urais wa CHADEMA,dkt Willbrod Slaa alipokuwa akiwahutubia mamia ya wakazi wa eneo la Mbauda mjini hapa.
Alisema kuhamishwa ghafla kwa mkurugenzi wa jiji, Raphael Mbunda kumetokana na shinikizo la Dk. Batilda baada ya malalamiko yake aliyoyawasilisha mara mbili kwa mkurugenzi huyo ambaye ndiye msimamizi wa uchaguzi jimbo la Arusha,akitaka Lema aondolewe kutokana na kutumia lugha za kumchafua, kuyatupilia mbali.
‘’ndugu zangu huyu mama ni mtu mbaya sana, amesababisha hadi mkurugenzi wa jiji amehamishwa ghafla kwa ajili yake ,alitumia mbinu ya kutaka mimi niondolewe ,amenishtaki mara mbili kwa msimamizi wa uchaguzi akisema eti namtukana ,nasema tena hafai akishtaki tena ‘’alisema Lema
Mbunda anadaiwa kukataa kumwondoa Lema kwenye kinyang’anyiro cha kampeni baada ya kuona hana hatia na kuishia kumwandikia barua ya karipio,hatua hiyo inadaiwa kumkera sana mgombea wa CCM na kuamua kupeleka malalamiko yake ngazi ya juu ambako pia aligonga mwamba,hali inayodaiwa na Lema kuwa aliamua kutumia cheo chake kuishinikiza wizara husika imng’oe na kumpa uhamisho wa lazima.
Mkurugenzi huyo ambaye alipewa siku tatu awe amekabidhi ofisi,amedumu katika halimashauri hiyo kwa muda wa miaka miwili akitokea halmashauri ya Meru wilayani Arumeru,amehamishiwa katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dodoma ambako hadi sasa hajapangiwa rasmi kazi ya kufanya, licha ya kupewa maelekezo ya kuripoti ofisini na kurudi nyumbani .
Aidha,taarifa zingine zimedai kuwa kilicho mng’oa mkurugenzi huyo ni utendaji mbovu wa kushindwa kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za halmashauri zilizokuwa zikutafunwa na wakuu wa idara baada ya kamati ya fedha za bunge kubaini mapungufu hayo na kuwasilisha mapendekezo kunakohusika.
Tayari nafazi ya Mbunda imechukuliwa na, Estom Chang’aa ambaye ametokea wizara ya TAMISEMI na utambulisho wake kwa wafanyakazi ulifanyika jana.
Gazeti moja la kila siku,limemnukuu waziri wa waziri wa nchi Ofisi ya waziri mkuu,Tawala za mikoa (TAMISEMI),Serina Kombani kuwa uhamisho huo ni wa kawaida na hauhusiani na mambo ya siasa ,hata hivyo waziri Kombani alisindwa kufafanua alipobanwa zaidi juu ya uhamisho kuwa wa ghafla bila hata kusubiri mshahara wake.
‘’uhamisho huo ni wa kawaida kama wengine anavyohamishwa ,kwa hiyo sioni kama ni habari’’alisema Kombani.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia