VYAMA VYA MIPIRA MANYARA VYATAKIWA KUFANYA UCHAGUZI ILI VIONGOZI WATAMBULIKE




MWENYEKITI wa Chama cha mpira wa miguu mkoani Manyara (MARFA) Charles Mngodo amevitaka vyama vya michezo vya wilaya za mkoa huo kufanya uchaguzi wao mapema ili kuwa na viongozi wanaotambulika kisheria.

Akizungumza na waandishi wa habari  mjini Babati,Mngodo alivipongeza vyama vya michezo vya wilaya za Simanjiro na Hanang’ kwa kufanya chaguzi zao na kupata viongozi wapya hivi karibuni.

Mngodo alisema kuwa vyama vya wilaya vya mkoa huo ambavyo hadi hivi sasa havijafanya uchaguzi wake ni Babati,Mbulu na Kiteto ambao wanatarajia kufanya uchaguzi wao hivi karibuni.

“Chama cha wilaya ya Kiteto (KIDFA) hakina matatizo kwani kinatarajia kufanya uchaguzi wake Januari 15 mwaka huu hii ni changamoto kwa vyama vingine ambavyo bado havijachagua viongozi wake,” alisema Mngodo.

Alisema chama cha mpira wa miguu wilayani Babati (BADFA) kinakabiliwa na changamoto kubwa ya viongozi wake kuwa na migogoro kila mara isiyo na tija hivyo wajipange kikamilifu kwa ajili ya kufanya uchaguzi na kumaliza migogoro.

Alisema migogoro kwenye michezo inasababisha kurudisha nyuma michezo kutokana na kushindwa kupanga mikakati ya maendeleo na kubaki kusuluhisha migogoro na malumbano yasiyo na maana wala faida.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

إرسال تعليق

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia