BARAZA LAUNGA MKONO UUNDWAJI WA KAMATI YA KUCHUNGUZA MAPATO NA MATUMIZI
Na Woinde Shizza ,Kondoa
Baraza la
madiwani Halmashauri ya wilaya ya Kondoa Vijijini Limeunga mkono kuundwa kwa
kamati ya kuchunguza taarifa ya mapato na matumizi ya Halmashauri hiyo ya mwezi
wa dec baada ya kuikataa kwenye kamati ya Uchumi na Fedha sanjari na madiwani
kukosa posho zao kwa miezi 11 sasa.
Akisoma kwenye
baraza hilo Taarifa ya kamati ya Fedha na Uchumi mwenyekiti wa Halmashauri hiyo
Gasper Mwenda Aliliambia kuwa kutokana na mapungufu yaliojitokeza wameonelea
kuunda kamati ndogo ambayo itapitia mapato na matumizi ya mwezi December na
kuirudishia kamati hiyo ambayo itawasilisha kwenye baraza hilo.
Amesema
suala hilo limejitokeza baada ya kamati hiyo kuirudisha ripoti ya matumizi na
fedha mara tatu ikiwa na mapungufu mbali mbali hivyo ilikuweza kujiridhisha
wameunda kamati ndogo ya kulifuatilia hilo kwa kina na wakimaliza watawasilisha
ripoti yao kwa kamati hiyo ambayo nayo itawasilisha kwa kwenye Baraza la
madiwani.
“Ukiangalia
Fedha za miezi ya Julai.ogasti,septemba mapato yamekuwa yakishuka toka million 13
hadi kumi hivyo mda huu tunaiomba kamati ndogo kulifuatilia hilo kwa kina
utaona hata madiwani wamekosa posho zao kwa miezi 11 sasa” alisema Mwenda
Suala hilo
ambalo diwani wa Viti maalum Asha Abdallah alisema kuwa japo limerudishwa
kwenye kamati ya fedha ambayo nayo imeunda kamati ndogo ya kupitia na
kujiridhisha bado changamoto ni kubwa kwani halmashauri imekuwa ikishuka
kimapato mara kwa mara na inakabiliwa na ukata mkubwa.
Nae
Mh.Ramadhan Bakari Akaitaka Halmashauri hiyo kujitathmini na kuimarisha mapato
yao ya ndani kwani imeshindwa hata kulipa mishahara ya wafanyakazi wake
wanaolipwa malipo ya ndani kwa kipindi kirefu sasa.
Amehoji
suala hilo akitanabaisha kuwa fedha zinazobaki kwenye mapato na matumizi ya
Halmashauri mbona hazielekezwi kwenye miradi ya maendeleo kama elimu maji na
Afya.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia