ADPA WAKUBALIANA KUPITIA UPYA NA KUREKEBISHA KATIBA NA MUONGOZO WA UMOJA HUO


 

Umoja wa nchi zinazozalisha almasi barani Afrika (ADPA) zimekubaliana kupitia upya na kurekebisha katiba na miongozo ya umoja huo kwa kuwa ile ya awali inepitwa na wakati.

Hayo yamesemwa leo na waziri wa madini nchini,Dotto Biteko katika mkutano wa ADPA unaondelea jijini Arusha.



Akizungumza na waandishi wa habari Waziri Biteko alisema kwamba tayari timu ya wataalamu imeshakamilisha nyaraka ambapo wataziwasilisha kwenye baraza la mawaziri ili ziweze kupitiwa .



Waziri Biteko alisema kwamba wamejiridhisha kwamba nyaraka hizo zinahitaji marekebisho ili ziweze kuendana na wakati.



“Leo zege halilali tunataka kuhakikisha tunakamilisha nyaraka za kuongoza ADPA ili kupitisha katiba iendane na wakati “alisema Biteko



Waziri Biteko alisisitiza kwamba umoja huo leo unataraji kukamilisha kazi ya kuajiri watendaji kwa kuwa waliokuwepo wametoa nchini Angola na wanafanya kazi kama hisani.



“Kazi tuliyonayo leo pia tuna agenda ya kuajiri watendaji kwani waliokuwepo wanatokea Angola na wanafanya kazi kama hisani hatuwezi kuwa na umoja wenye nguvu wakati una watendaji wa kuazima “alisisitiza Waziri Biteko



Hatahivyo,waziri Biteko alisisitiza kwamba mbali na umoja huo kuwa na wanachama 19 tayari kuna nchi 6 barani Afrika zimeomba kujiunga na mchakato bado unaendelea.


About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia