JINSI MABADILIKO YA TABIA NCHI YANAVYO MUHATHIRI MWANAMKE
Na Woinde Shizza , ARUSHA
Lesika Simoni akiwa kama mama wa familia anaeleza zaidi namna anavyoathirika na mabadiliko ya tabia nchi hususa ni katika eneo analoishi ambapo anadai kuwa ukame uliokuwepo wa muda mrefu umemsababishia hata uchumi wake kuyumba.
Pia amekuwa akipata tabu ata ya kupata maji ya kunywa yeye na familia yake ,mifugo na hata ameshidwa kufanya kilimo kutokana na ukame
Anaenda mbali zaidi na kusema muda mwingine anashidwa hata kutimiza majukumu yake kama mlezi anae hudumia familia kwa karibu zaidi mabadiliko haya humfanya kuwa katika mazingira hatari zaidi wakati wa ukame unapotokea kama kipindi hichi.
Changamoto zipi zinamkumba katika kipindi hichi?
Anaenda mbali zaidi na kubainisha kuwa kuna matatizo mbalimbali ambayo yamemkumba kutokana na mabadiliko haya ambapo alisema kitu kikubwa kinacho mtesa ni ukame uliopo katika kijiji chao
Mbuzi wakiwa wanakula vumbi na mabaki ya majani yaliyokauka kutokana na ukame
Ukame
Amebainisha kuwa katika kijiji chao wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa maji safi na salama ya kunywa wao pamoja na familia yake ambapo anafafanua zaidi na kueleza kuwa imefikia hatua wanalazimika kununua maji kutoka mji wa Arusha mjini karibia kilometa 37 ambayo yanafutwa na mmoja wa wananchi na kuyaleta kijiji hapo ambapo wanauziwa kwa shilingi 1000 kwa ndoo moja ya lita 20
“mimi kiukweli mabadiliko haya ya tabia nchi yameniathiri kwa kiasi kikubwa kwanza katika swala la maji sisi hapa kijijini kwetu hatuna mradi wowote wa maji tulikuwa tunategemea maji kutoka katika mto Nanja ule pale unaouona lakini kama unavyoona mto huu umekauka na mbali ya kukauka , maji haya kidogo unayoyaona hayafai ata kupikia chakula kwani ukipikia ugali unabadilika badala ya kwa na rangi nyeupe unakuwa wa kijani na pia unakuwa na ladha mbaya ya magadi ambapo ukipikia chakula hakifai hata kuliwa”alisema
Ameathirikaje katika kilimo ?
Anaeleza kuwa kwa upande wa kilimo ameathirika sana kwa kuwa awali alikuwa anategemea kulima mazao kama mahindi na maharage lakini kutokana na ukame uliopo ameshindwa kulima
“uku kwetu pia tumezoea kulima kwa msimu mmoja lakini msimu huo ulikuwa unatusaidia kupata kilimo ambacho tuta uza mazao na hapo hapo tutapata chakula kwa ajili ya watoto lakini kinachoniumiza nikiangalia sasa hata hicho chakula tu chakuwapa watoto atupati apa kwetu gunia la mahindi limefika hadi shilingi laki na nusu na ukiangalia mazingira yetu ni ngumu kununua watoto wanakufa njaa ,tuliomba serikali wakatupatia mahindi kwa bei nafuu ya shilingi elfu 80000 lakini pia tunashindwa kwenda kuyachukuwa kwakuwa hatuna ela ya kununua na hata kusafirisha kwa iyo mimi kama mimi naweza sema nimeathirika sana na haya mabadiliko yatabia nchi naomba nimuombe Rais aangalie tu namna ya kutusaidia “alifafanua
ASASI ZISIZO ZA KISERIKALI ZAONGEA ?
Mkurugenzi wa Shirika la ustawi wa wanawake na watoto (Mimutie women organization )MWO Mery Mushi anaeleza zaidi baadhi ya athari za mabadiliko hayo ya tabia nchi kwa mwanamke
Anaeleza kuwa wanawake huwa katika hatari zaidi za kuathiriwa na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi, na haswa katika mazingira ya umasikini, kutokana na uwezo wao mdogo wa kukabiliana na majanga kama vile kiangazi na mafuriko
Mabadiliko ya tabia nchi yanavyowaathiri wanawake yanawaumiza kwa namna kubwa kwa kuwa ukiangalia wanawake ndio wanapata shida kubwa pale wanapokuwa wenyewe ni watafutaji haswa katika nyakati hizi ambazo asilimia kubwa ya wanawake wamekuwa ni watafutaji wa familia zao hasa kwa jamii za pembezoni pamoja na wale waliopo mjini
Tukiangalia kwa jamii za pembezoni tunaona kwamba wao wanaathirika zaidi wanawake wa vijijini kwa mfano kwa kipindi hichi kumetokea wimbo la wafugaji kuhama maeneo yao na wanavyohama na mifugo imekuwa nayo inaondoka sasa inapo ondoka mifugo wanaondoka na vijana wa kiume au watoto wa kiume lakini pia ile mifugo ilikuwa ikikaa nyumbani ilikuwa inawanufaisha wa njia nyingine aidha ya kuwapatia maziwa ambapo yale maziwa walikuwa wanaweza kusaidia Kwa kutumia kwa kuwapa watoto au kwa kuuza kwenye jamii zao
Bei kuendelea kuwa juu kutokana na mabadiliko ya tabia nchi
-Mvua zimechelewa kunyesha hivyo zimepelekea bidhaa nyingi au mazao mengi kutoweza kupatikana kiurahisi kwa hiyo hii imechangia kwa kiasi kikubwa kipato cha mwanamke kuanza kushuka kwa sababu wanakosa munkhari ya kuweza kufanya biashara zao kutokana na namna ambavyo mitaji yao ilivyokuwa mwanzo na sasa hivi inashuka kutokana na vile ambavyo mitaji ina kuwa labda ilikuwa mtu anamtaji wa elfu 50000 lakini bidhaa zimeenda kuongezeka bei sokoni kwa hiyo mtaji wake aliokuwa nao hauwezi tena kununua vitu alivyokuwa akiviitaji hivyo anakuwa ajatimiza malengo yake aliyojiwekea .
SERIKALI IFANYE NINI ILI JAMII HIZI KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI
-Jamii za kifugaji zipewe uelewa wa nini cha kufanya pindi janga hili la mabadiliko ya tabia nchi linapotokea ambapo wanafunzi wanao soma vyuo vya kilimo pindi wanapotoka vyuoni wapite katika jamii hizo na kutoa elimu kwa wananchi ya nini kifanyike mfano ukame ukitokea ,mafuriko na nk.
-Mabadiliko haya yapoadhiri wananawake kwa namna moja ama nyingine serikali inatakiwa iangalie namna gani itaweza kuwawezesha kiuchumi ili waweze kuendelea na shughuli zao za kuwaingizia kipato mfano kuwapatia mikopo ambayo itawasaidia kuendeleza biashara zao ili waweze kufanikisha kazi zao za kila siku
WAANDISHI WA HABARI WAFANYE NINI
-Ili kukabiliana na mabadili haya ni wajibu wa kila mwaandishi wa habari na mtangazaji kutumia elimu yake pamoja na kalamu yake kuelimisha uma kuhusiana na mathara ya ukataji miti hovyo na namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi pindi yanapo tokea
WANANCHI WAFANYE NINI IILI KUKABILIANA NA MABADILIKO HAYA
-Ni wajibu wa wananchi kutambua mathara ya uchafuzi wa mazingira ambayo yanapelekea kuongezeka kwa mabadiliko ya tabia nchi
-Ni vyema wananchi wakajitaidi kupanda miti kwa wingi ,kutokata miti ovyo ili kuondokana na janga hili
-Kila mwananchi awe balozi wa mwenzake wa kumueleza madhara ya mabadiliko ya tabia nchi ili kila mmoja ayajue
TAKWIMU ZA UMOJA WA MATAIFA ZINASEMAJE?
Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha asilimia 80 ya watu wanaolazimika kuhama makazi yao kutokana na mabadiliko ya tabia nchi ni wanawake.
Majukumu yao kama walezi na wanao hudumia familia kwa karibu zaidi huwafanya kuwa katika mazingira hatari zaidi wakati wa mafuriko na ukame unapotokea.
Makubaliano ya mjini Paris mwaka 2015 yaliweka kipaumbele maalum cha kuwawezesha na kutambua kwamba wanawake huathiriwa kwa kiasi kikubwa zaidi katika jamii kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.
Wakati wa kiangazi wanaume wanaenda mjini na kuwaacha wanawake vijijini kuangalia jumuiya, Hivyo wanawake wanalazimikia kufanya kazi zaidi ili kutunza watoto bila msaada wowote.
Lakini sio wanawake wa maeneo ya vijijini peke yake ndio wanaathirika.
Duniani kote wanawake wanaathirika zaidi kutokana na umaskini na kutokuwa na uwezo mkubwa zaidi ya wanaume katika masuala ya kiuchumi hivyo hali ambayo huwafanya washindwe kujikwamua kutoka katika majanga ambayo yanaharibu miundombinu ,ajira na makazi yao.
Aidha zaidi ya nusu ya familia zinazo ishi mjini zinatunzwa na wanawake.
Wakati Katrina ilipotokea mwaka 2005,wanawake na watoto ndio waliathirika zaidi katika upande wa makazi ,afya na hata walikumbana na unyanyasaji wa kijinsia kama kubakwa.
Vile vile mabadiliko ya tabia nchi huathiri shughuli za kibinadamu, athari za hali ya hewa na maafa yanayotokea katika jamii husika huwa na athari tofauti kwa wanawake na wanaume.





0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia