Mkurugenzi wa kampuni ya BIMO Media , Bertha Ismail akisoma risala katika ufunguzi wa maadhimisho ya ufunguzi wa michuano ya Nyerere Cup 2015 yaliyokuwa yakitimua vumbi katika uwanja wa Stedium jijini Arushaambapo pia yataambatana na mashindano ya kila mwaka ya kielimu ya uandishi wa insha,makala pamoja na uchoraji picha juu ya masuala ya utalii kwa wanafunzi wa shule za msingi 25 zilizopo Arusha yaliyoandaliwa na kampuni ya BIMO Media
Mgeni
rasmi Afisa Elimu jiji la Arusha kwa shule za sekondari Josephat
m.Ntabindi akiongea na vyombo vya habari pamoja na wanamichezo chini ya
umri wa miaka 13,alisema kuwa mashindano hayo ni kwa ajili ya kumuenzi
hayati baba wa taifa Mwl Julias Nyerere ambaye pia alikuwa mstari wa
mbele katika kuhamasisha michezo.
Mgeni
rasmi ambaye Afisa Elimu jiji la Arusha kwa shule za sekondari Josephat
M.Ntabindi akisalimiana na wachezaji kabla ya mechi ya TIMU ya Maafande wa JKT Oljoro ya jijini Arusha na timu ya AFC Arusha katikaufunguzi wa michuano ya Nyerere Cup 2015.
Watoto wenye chini ya umri wa miaka 13 wakifanyiwa mahojiano ,aliyeshika maiki ni mmiliki wa jamiiblog Bi.Pamela Mollel
TIMU
ya Maafande wa JKT Oljoro ya jijini Arusha inayoshiriki ligi daraja
lakwanza imeshindwa kuonyesha makali mbele ya wadogo zao timu
ya AFC Arusha inayoshiriki ligi daraja la pili baada ya kutoka suluhu
ya bao 1-1 katika ufunguzi wa michuano ya Nyerere Cup 2015.
Mchezo
huo uliofanyika katika uwanja wa Sheikh AmrI Abeid ,uliiwashuhudia
maafande hao wa Oljoro wakianza kucheka na nyavu za AFC baada ya
kujipatitia bao lake kupitia kwa mchezaji Swalehe Idd alilofunga kwa
njia ya Penalti mnamo dakika ya 58, iliyosababishwa na mabeki wa timu
pinzani kunawa mpira katika eneo la hatari.
Vijana
wa AFC walionyesha juhudi zao kwa kulishambulia lango la Oljoro ambapo
walifanikiwa kusawazisha bao mnamo dakika ya 88 kupitia kwa mshambuliaji
wao Wandima Malechela baada ya kuachia shuti kali lililokwenda moja kwa moja vyavuni.
Mashindano hayo yameandaliwa na kampuni ya BIMO Media yakiwa na kauli mbiu ‘Uchaguzi wa Amani 2015,ndio
taifa moja kwa maendeleo ya utalii nchini’ yatazishirikisha pia timu za
watoto chini ya miaka 13 ambao watachuana vikali ili kuweza kumpata
mshindi ambaye atatangazwa siku ya kilele tarehe 19 mwezi huu.
Akifungua
mashindano hayo Afisa Elimu jiji la Arusha kwa shule za sekondari
Josephat m.Ntabindi alieleza kuwa mashindano hayo ni kwa ajili ya
kumuenzi hayati baba wa taifa Mwl Julias Nyerere ambaye pia alikuwa
mstari wa mbele katika kuhamasisha michezo.
“Michezo hii inawakutanisha vijana hawa wakiwa na uwezo wao tofati ambapo pia yatawajengea urafiki na uhusiano mzuri baina yao vile vile yatawasidia kuweza kuimarisha vipaji vyao vitakavyotumika
katika kuandaa taifa lililo na vijana wenye uwezo mzuri na pia
yatahamasisha utalii kwani mkoa huu una vivutio vingi.”alieleza
Ntabindi.
Naye mkurugenzi wa kampuni ya BIMO Media , Bertha Ismail alisema maadhimisho hayo yataambatana na mashindano ya kila mwaka ya ki- elimu ya uandishi wa insha,makala pamoja na uchoraji picha juu ya masuala ya utalii kwa wanafunzi wa shule za msingi 25 zilizopo Arusha.
“ Lengo ni kuhamasisha uchaguzi wa mwaka huu kufanyika kwa amani vile vile kuhamasiha watu kuhudhuria hifadhi za utalii zilizoasisiwa na Mwl Nyerere na tunategemea Zaidi ya wanafunzi 700 watashiriki katika shindano hilo la isha.”ismail alifafanua.
Timu
za nyota academy,Future Stars,Kijenge Youth,Rolling Stone,Young Life na
palloti zitachuana na washindi watakabidiwa zawadi mbalimbali ikiwemo
vikombe na fedha.