TIMU ya Rafiki fc ya wilayani Arumeru imefanikiwa kutwaa ubingwa wa kombe la Sethi
Bewnjamini lililofikia tamati jana (jumapili) baada ya kuwafunga wapinzani wao
timu ya Pande za home kwa kuwafunga kwa jumla ya penalti
6-5.
Mashindano
hayo ya kombe la Seth Benjamin yalianza kutimua vumbi mwezi Julai na kufikia
tamati mwezi septemba mwaka huu .
Mabingwa
hao wa Rafiki fc waliweza kukabithibiwa
zawadi ikiwemo kombe na kitita cha shilingi laki tano ,huku mshindi wa
pili ikiwaendea timu ya Pnde za Home kwa kuzawadiwa seti ya jezi
na mipira miwili na mshindi wa tatu kuwa ni
Chachyi SC baada ya kuwafunga timu
ya Dulluti kwa jumla ya mabao 3-2.
Jumla
ya timu 14 kutoka wilaya ya Arumeru zilionyesha ushindani wa aina yake katika
kuwania kombe la Seth Benjamini
aliyekuwa muasisi wa Azimio la
Arusha ambaye alifariki mwaka 1967.
Timu hizo ni
ST.Domingo , Manyata, Duluti,Rafiki, Railway SC, Maji ya chai,
Embaseni,Usa Star,Meru Worrious, Pande za home ,Chemchem, Magadini ,Waya mkali na Chackyi SC zinachuana vikali katika
mashindano hayo) yalifanyika katika viwanja vya Ngaresero ambavyo hizi sasa vinajulikana kama viwanja
vya kumbukumbu ya Seth Benjamini .
Akisoma
Risala kwa mgeni rasmi,Mratibu wa mashindano hayo Moody Hassan Orondi, alisema
hayati Sethi Benjami ni alikuwa miongoni mwa mashujaa ambao wataendelea
kukumbukwa kwani alikuwa ni mmoja wa shujaa aliyeunga mkono azimio la Arusha kwa matembezi ya miguu.
“Kwa
kweli tutamkumbuka sana kwani alikuwa shujaa aliyeonyesha uzalendo mkubwa kwa kupiga vita Rushwa ,ufisadi, ambavyo hadi
leo ni tatizo katika nchi yetu hivyo tutaendelea kuadhimisha kkila mwaka na
pia uwanja huu tumeupa heshima kwa kuuita
uwanja wa kumbukumbu wa Seth Benjamini”alisema Orondi .
Orondi
aliongeza kuwa Kwa mara ya kwanza
mashindano hayo yamefanyika ili kuweza kumkumbuka mwasisi huyo
ambaye anakumbukwa kama shujaa ,alikuwa
akisafiri kutoka Arusha kwa matembezi
kuelekea Dar es salaam ambapo
alipofika eneo la maji ya chai ,Usa river alizidiwa gafla na kupoteza mwezi
julai mwaka 1967.
Mgeni
rasmi katika michuano hiyo Inspector Charles
Mbawala ambaye ni makamo mkuu wa
upelelezi wilaya ya Arumeru aliwasihi vijana waendelee kuipenda michezo kwani
itawafanya wajijengee mazingira mazuri ya kukuza vipaji vyao
na kusema jeshi la polisi wilyani
Arumeru linaandaa mashindano ambayo yatashirikisha timu mbalimbali za
mpira wa soka.
Mashindano
hayo yaliandaliwa na familia ya marehemu kwa kushirikiana na diwani anayemaliza
mda wake wa kata ya Usa RIVER (CCM) Zubery Simbano
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia