Wananchi wa Mtaa wa Majengo Chini, Kata ya Sombetini wakimsikiliza
kiongozi wa Tawi la CCM Sombetini akikabidhi bango la tawi lao kwa Katiu wa
CHADEMA Mkoa wa Arusha, Mh Kalist Lazaro katika mkutano wa kampeni kumnadi
mgombea udiwani Kata ya Sombetini kupitia CHADEMA Mh Ally Bananga.
Mgombea Udiwani Sombetini akijinadi kwa wananchi kuomba kuchaguliwa tena baada ya kuwaongoza kwa mwaka mmoja na nusu katika Kata ya Sombetini Jijini Arusha. Mkutano huo ulifanyika jana jioni katika Mtaa wa Majengo Chini, eneo ambalo liko chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa Mtaa atokanaye na CHADEMA Godfrey Kitomari aliye kwenye msuguano mkali na Bananga baada ya kuzidiwa katika uteuzi wa mgombea udiwani ndani ya chama hicho.
Kitomari analalamikizwa kufanya kampeni hasi dhidi ya mwanachama mwenzake katika Kata hivyo, lakini akihutubia mkutano huo Katibu wa CHADEMA Mkoa alieleza wanachama wa chama chake kutopoteza muda na waliosaliti au ambao wana dhamira zakusaliti kwasababu mabadiliko hayasubiri mtu yeyote. Alienda mbali zaidi na kutolea mfano wa viongozi wakubwa wa UKAWA kama Prof Lipumba na Dr SLaa walivyosaliti lakini umma uliwapuuza ndani ya muda mfupi.
Kiongozi mwakilishi wa CHADEMA idara ya intelijensia Taifa alipata wasaa
wa kusalimia wananchi wa Sombetini mkutanoni hapo na kuwaombea kura
wagombea wote wa Udiwani (Bananga) Ubunge (Godbless Lema) na Urasi
(Lowassa)
Alitumia nafasi hiyo pia kuwatoa hofu wananchi kuwa uchaguzi utakuwa wa amani na hakutakuwa na vurugu ya aina yeyote na kwamba wameshakubalina na Tume ya Uchaguzi, Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama kuwa matokeo yote ya kuanzia udiwani, ubunge na urais yatabandikwa kwenye mbao za matokeo mara baada ya kuhesabiwa ili kuepusha nchi na hatari ya kuvurugika amani.
Alitumia nafasi hiyo pia kuwatoa hofu wananchi kuwa uchaguzi utakuwa wa amani na hakutakuwa na vurugu ya aina yeyote na kwamba wameshakubalina na Tume ya Uchaguzi, Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama kuwa matokeo yote ya kuanzia udiwani, ubunge na urais yatabandikwa kwenye mbao za matokeo mara baada ya kuhesabiwa ili kuepusha nchi na hatari ya kuvurugika amani.
Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha, Mh Kalisti Lazaro akihutubia mkutanoni
hapo ambapo alimpiga vijembe mshindani wa Godbless Lema, ambaye ni mgombea
Ubunge wa Arusha Mjini kupitia CCM Philemon Mollel almaarufu Monaban kuwa
anawadanganya wanawake kuwapa mikopo wakati yeye mwenyewe anadaiwa na bank
zaidi ya bilioni 3.
Lazaro “Bush” ni mgombea Udiwani kata ya Sokoni I lakini alidai hana mtu wa kushindana naye ndio maana anashiriki kamapeni maeneo mengine.
Lazaro “Bush” ni mgombea Udiwani kata ya Sokoni I lakini alidai hana mtu wa kushindana naye ndio maana anashiriki kamapeni maeneo mengine.
Baadhi ya wagombea udiwani wa CHADEMA kwa Jimbo la Arusha Mjini
wakisalimia wananchi kwa pamoja baada ya kutambulishwa katika mkutano
huo
Ally Bananga akisimulia baadhi ya amambo aliyotekeleza kwa kipindi cham
mwaka mmoja na nusu aliokuwa Diwani wa Sombetini na kueleza mafanikio yake
kwa utatuaji kero ya madawati kwa shule za msingi, uboreshaji miundo mbinu
na ujenzi wa madarasa kwa ajili ya watoto kupata pa kusomea. Katika Mtaa wa
Majengo alisimulia namna kero ya mtaro wa maji inavyosumbua na kuahidi
kuendelea pale alipoishia kutafuta ufumbuzi kamili kwa kuwashirikisha
TANROADS ambao walidaiwa kuwa wahusika wakuu wa mtaro huo.
Kiongozi wa Tawi la CCM Sombetini akitoa maelezo kwa wnanchi na kueleza
kuwa wamehamia CHADEMA tawi zima ili kukimbizana na kiu ya Mbadiliko
waliyonayo watanzania wengi nchini. Baadae alikabidhi bango lao na kuruhusu
wanachama kulitumia wapendavyo. Baadhi walianza kuligombania na kutaka
kulichoma moto hapo hapo lakini viongozi wa CHADEMA waliwazuia.
Wananchi wakigombana kulichanchana bango la wanaCCM waliohamia CHADEMA
jana
tabasamu la furaha baada ya kuhamia CHADEMA
Mgombea Udiwani Sombetini Ally Bananga na Katibu wa CHADEMA Mkoa wa
Arusha Kalist Lazaro wakiondoka eneo la mkutano baada ya kuahirishwa na
kusindikizwa na umati wa watu
Timu ya mgombea Udiwani Bananga ikiondoka eneo la mkutano