Siku
chache baada ya Baraza la Sanaa la Tanzania(Basata) kulifungulia
shindano la Miss Tanzania mrembo anayeshikilia taji hilo kwa sasa,Lilian
Kamazima amefunguka na kupongeza uamuzi huo na kudai kwamba kufunguliwa
kwake kumefungua ndoto na ajira mbalimbali hususani kwa wasichana
nchini.
Hatahivyo,mrembo
huyo amesisitiza ya kwamba Tanzania inabidi “ikaze” kujiandaa na
mashindano ya dunia yanayotaraji kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Akihojiwa
na gazeti hili kwa njia ya simu akiwa jijini Dar es salaam mrembo huyo
alisema kwamba bado hajapata taarifa rasmi kutoka katika kampuni
inayoyasimamia mashindano hayo lakini amefurahishwa na uamuzi huo.
“Nimejisikia
vizuri sana unajua hapo awali nikiongea na wasichana walikuwa
wakiniuliza vipi kuhusu ndoto na matarajio yao”alisema Kamazima
Hatahivyo,alisisitiza
kwamba hivi karibuni anataraji kukutana na Rais Jakaya Kikwete katika
kikao maalumu na atazungumza na vyombo vya habari mara baada ya kikao
hicho bila kufafanua nini watakwenda kujadili.
Naye,wakala
wa mashindano ya Miss Tanzania kanda ya Kazkazini,Faustine Mwandago
kupitia kampuni yake ya Mwandago Investment alitoa maoni yake na kusema
kwamba anatarajin mashindano hayo yatakuwa bora hapo mbeleni endapo
masharti ya Basata yakitekelezwa kikamilifu.
Hatahivyo,baba
mzazi wa mrembo wa taji la Miss Tanzania mwaka huu,Deus Kamazima kwa
upande wake alitoa maoni yake na kusema kwmaba mbali na kufurahishwa na
uamuzi huo lakini alisema kwamba kufungiwa kwa shindano hilo kumeathiri
ajira mbalimbali nchini.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia