Mgombea Ubunge wa Jimbo la
Mufindi Kusini Ndugu Mahmoud Mgimwa akipiga push up mbele ya wakazi wa
Mafinga waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni wa kumnadi
mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli ambaye
anashuhudia
tukio hilo katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vyaWambi mjini
Mafinga mkoani Iringa na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa
wananchi.
Dk. John Pombe Magufuli
amewaambia wakazi hao wasihadaike na maneno ya kisiasa yanayotolewa na
vyama vingine kuwa nchi ya Tanzania haijapiga hatua ikiwa chini ya
utawala wa CCM wakati maendeleo yanaonekana wazi na nchi inazidi kusonga
mbele kwa mambo mengi ikiwemo amani na utulivu wa nchi.PICHA NA MICHUZI
JR-IRINGA
Waziri
Mkuu mstaafu, Samuel Malecela akitangaza wasifu wa Dk Magufuli na
kwamba ndiye anayefaa kuchaguliwa kuwa rais tofauti na mgombea wa Ukawa,
Edward Lowassa.
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
akiwahutubia wakazi wa Chimala,Mbarali mkoani Mbeya alipokuwa akielekea
mkoani Iringa kuendelea na kampeni zake.
gombea Urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama
cha CCM Dkt John Pombe
Magufuli akionesha hisia zake mara baada ya kuonana uso kwa uso na Kada
Mkongwe wa chama cha CCM Ndugu
Samwel Malecela mjini Mbarali kabla ya kuwahutubia wananchi kwenye
mkutano wa kampeni
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe
Magufuli akizungumza jambo na Kada Mkongwe wa chama cha CCM Ndugu Samwel
Malecela mjini Mbarali kabla ya kuwahutubia wananchi kwenye mkutano wa
kampeni,huku Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Ndugu Bulembo akifuatilia
kwa
makini
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
akiwahutubia wananchi wa
Rujewa mjini katika viwanja vya Barafu mjini Rujewa,wilaya ya Mbarali
mkoani Mbeya leo Septemba 27 kwenye
mkutano hadhara wa kampeni.
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa
Rujewa mjini wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya leo Septemba 27 kwenye
mkutano hadhara wa kampeni.
Mgombea
Ubunge wa
jimbo la Makambako Ndugu Deo Sanga a.k.a Jah People akimuombea kura
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa hadhara
wa kampeni uliofanyika mjini Ilembula leo Septemba 27 mkoni
Mbeya
Mgombea
Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge wa jimbo
la Wanging'ombe Injinia Gerson Rwenge,katika mji wa
Ilembula
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha
Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasili kwenye mjini Makambako
kwenye uwanja wa Polisi Mwembetogwa mkoani Iringa leo Septemba 25 kwenye
mkutano wa
hadhara wa kampeni.
wakazi
wa Makambako wakishangilia wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe
Magufuli alipokuwa akipanda jukwaani kwa kuruka ruka kuonesha yuko fiti
kuwatumikia wananchi kwa namna yoyote ile.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Wazazi na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa Ndugu Abdalah
Bulembo akiwahutubia wakazi wa Makambako kwenye mkutano wa kumnadi
mgombea urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli leo Septemba 27 mkoani
Iringa
Dkt Magufuli akiwasalimia wananchi wa Makambako
kabla ya kuanza kuwahutubia na kuwaomba kura
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha
Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa
Makambako gombea Ubunge wa jimbo la Makambako Ndugu Deo Sanga
wakiwaimbisha wananchi wa Mafinga
katika uwanja wa Polisi Mwembetogwa mkoani Iringa leo Septemba 25 kwenye
mkutano wa
hadhara wa kampeni.
Wananchi
wa mji wa Makambako wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha
Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake na
kuwaomba wajitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura Oktoba 25 kwa kumpiga
kura ya ndio na hatimae aibuke mshindi kwa nafasi ya
Urais
Mmoj
wa Waangalizi wa Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka
huu,akifuatilia mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli
mjini Makambako jioni ya leo Septemba 27 mkoani Iringa
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha
Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mgombea Ubunge wa jimbo
la Makambako Ndugu Deo Sanga wakiwaiambisha wananchi wa Mafinga
katika uwanja wa Polisi Mwembetogwa mkoani Iringa leo Septemba 25 kwenye
mkutano wa
hadhara wa kampeni.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha
Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Mafinga
katika uwanja wa Mafinga mkoani Iringa emba 25 kwenye mkutano wa
hadhara wa kampeni.