Na Woinde Shizza,Arusha
Zaidi
ya wamiliki 800 wa migod ya madini mbalimbali nchini na wenye leseni za
uchimbaji zaidi ya 4000 wameanza kusajiliwa kwenye mtandao na ofisi
ya kanda ya kaskazini ya madini kuweza kupata idadi yao na kuweza
kuendana na teknolojia ya mawasiliano inayokuwa kwa kasi na kuweza
kupata takwimu mbalimbali kuhusu madini yao.
Hayo
yameelezwa leo na Kaimu Kamishna msaidizi wa madini wa kanda ya
kaskazini Bw,Alex Magayane wakati wa mahojiano na waandishi wa habari
yaliyofanyika katika ofisi za kanda hiyo zilizoko katika halmashauri ya
jiji la Arusha ,mkoani Arusha .
Hata
hivyo alisema kuwa lengo hasa la kusajili wachimbaji hao wa madini
kuweza kuwaingiza kwenye mtandao ambapo kazi zao zitafanyika kwa urahisi
kupitia technolojia hii mpya na kuweza kurahisisha utendaji wakazi yao
na wachimbaji na haswa ofisi ya madini ,na kupata huduma kwa haraka
popote pale walipo ili kuwapunguzia usumbufu ambao awali ilikuwa
inamlazimu mchimbaji pindi akihitaji huduma yoyote ya ofisi mpk aende
ofisi ya kanda lakini kwa sasa itamsaidia mchimbaji huyo kupata taarifa
zote kwenye mtandao kupitia huduma mbalimbali zikiwemo simu za kiganjani
,mitandao ya internet na huduma mbalimbali.
Hata
hivyo alisema kuwa kupitia zoezi hilo la usajili litawasaidia hata
kuongeza ufanisi wakazi zao na kumwezesha mchimbaji huyo kuweza kupata
takwimu ama taarifa zozote anazohitaji juu ya masuala ya madini na hata
bei za madini na bei elekezi za siku hiyo.
Kamishna
Bw,Alex huyo mbali na jitihada mbalimbali za kuboresha huduma kwa
wachimbaji hao kuwekuwepo na changamoto kubwa sana hususani upande
wawachimbaji hao ambapo wengi wao wamekuwa hawajui namna ya kutumia
mitandao hali hata kuweza kufungua email ambayo imekuwa ikikwamisha
jitihada mbalimbali za kuweza kuboresha huduma hizo za kuwahudumia kwa
kupitia mitandao.
Na
amewataka wachimbaji hao kuweza kutoa ushirikiano wa kuweza kujitokeza
kwa wingi kujiandikisha na kuqweza kutambuliwa na ofisi yake na kuweza
kuwarahisishia kupata huduma wazitakazo kwa haraka zaidi na kuweza
kuongeza tija na ufanisi katika biashara zao za madini.
Hata
hivyo amewataka wachimbaji hao kuweza kuhakikisha kila mmiliki wa mgodi
anahakikisha anasajiliwa kwani faida zab usajili nikubwa kulinganisha
kuwa nje wa mtandaoa kwani pindi kunapohiaji kuweza kuwapa taarifa
wachimbaji hao njia rahisi ya kuwapata kwa pamoja nikwenye mtandao
kupitia usajili huo.
Aidha
zoei hilo litadumu mpaka mwisho wa mwezi desemba mwaka huu ili kuweza
kuhakikisha wachimbaji wote wenye sifa za kupata leseni wameandikishwa
na kurahisisha ufanisi na utekelezaji wa kazi zao na kupunguza mlolongo
wakuenda katika ofisi za kamnda hiyo ili kuweza kupata huduma.