WATANZANIA 500,000
wanatarajiwa kutembelea mbuga zote 16 za hifadhi za taifa mwaka huu ikiwa ni
hatua ya kuimarisha na kukuza utalii wa ndani ambapo watajionea vivutio
mbalimbali vilivyomo ndani ya hifadhi hizo.
Hayo yameelezwa leo na
Meneja uhusiano wa shirika la hifadhi za taifa, Tanapa,Pascol Shelutete, makao
makuu ya TANAPA, jijini ,Arusha, alipokuwa akizindua hatua ya mwisho ya kampeni
maalumu ya miezi sita ya kuhamasisha Watanzania kutembelea
hifadhi ili kujionea vivutio kwenye hifadhi wanazopakana nazo ili
kuimarisha utalii wa ndani
Kampeni hiyo ni Makakati
maalumu uliobuniwa na Tanapa, unaotoa hamasa kwa watanzania kutembelea
mbuga za hifadhi zilizopo karibu na maeneo yao kwa gharama nafuu hasa siku za
mwishoni mwa wiki na hivyo kuwapunguzia matumizi ya fedha wanazotumia kwenye
starehe na badala yake wazitumie kutembelea hifadhi .
Meneja uhusiano wa
Tanapa, Shelutete, amesema kuwa kadiri miaka inavyozidi kusonga
mbele mwamko wa watanzania kutembelea mbuga za hifadhi unaongezeka, ambapo
mwaka 2013 watanzania 362,217, walitembelea hifadhi zote 16 nchini, na mwaka
2014 watanzania 427,258 wametembelea mbuga hizo .
Amesema hatua ya mwisho
ya uzinduzi wa kampeni hii inafanyika mkoani Arusha,ambao unapakana na mbuga za
hifadhi za Arusha, Ziwa Manyara na Tarangire,na kampeni hiyo itadumu kwa muda
wa miezi 6 na itahitimishwa Desemba mwaka huu.
Kauli mbinu ya kampeni
hiyo ni “Tembelea hifadhi uzwadike , akatoa wito kwa watanzania kubadili
mitizamo kwa siku za mwishoni mwa wiki zitumike kwa ajili ya kutembelea hifadhi
badala ya kuzitumia kwa ajili ya starehe ambazo zinatumia fedha nyingi.
Uzinduzi huo
umeshirikisha wakuu wa Idara za utalii wa hifadhi za Tarangire, Ziwa Manyara na
hifadhi ya Arusha, pamoja na wadau ambao ni Chama cha waongoza utalii nchini
TATO,ambao kwa pamoja wameelezea manufaa ya kutembelea hifadhi za taifa na
sanjari kutatolewa zawadi mbalimbali kwa watanzania watakaotembelea hifadhi hizo.