|
Baadhi ya wana CCM
na wananchi wakiwa wamefurika katika Viwanja wa Jitegemee Mjini Muheza
ambapo mgombea mwenza nafasi ya urais CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alifanya
mkutano wa kampeni leo. |
|
Baadhi ya wana CCM na wananchi wakiwa wamefurika
katika Viwanja wa Jitegemee Mjini Muheza ambapo mgombea mwenza nafasi ya
urais CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alifanya mkutano wa kampeni
leo. |
|
Mgombea mwenza wa
urais kupitia CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan akihutubia umati wa wanaCCM na
wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wake wa kampeni uliofanyika viwanja
vya Usagara Tanga Mjini leo. Idadi kubwa ya wananchi walihudhuria mkutano
huo hadi wengine kuzimia kutokana na msongamano. |
|
Baadhi ya wana CCM na wananchi wakiwa wamefurika
katika Viwanja wa Jitegemee Mjini Muheza ambapo mgombea mwenza nafasi ya
urais CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alifanya mkutano wa kampeni
leo. |
|
Mjumbe wa Kamati ya
Kampeni za CCM Kitaifa, Bi. Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi kwenye
moja ya mikutano ya kampeni za CCM timu ya mgombea mweza iliyofanyika
mkoani Tanga leo. |
|
Baadhi ya vijana
wakiwa wamepanda juu ya gari ili kumsikiliza mgombea mwenza wa CCM, Bi.
Samia Suluhu Hassan katika Jimbo la Mkinga. |
|
Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan
akiwa amesimamishwa na wananchi njiani alipokuwa akielekea katika Jimbo la
Mkinga kufanya mkutano wa kampeni. |
|
Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan
akiwa amesimamishwa na wananchi njiani alipokuwa akielekea katika Jimbo la
Mkinga kufanya mkutano wa kampeni. |
|
Sehemu ya wanaCCM na
wananchi ikiwa imemsimamisha barabarani mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia
Suluhu kumsikiliza alipokuwa njiani kuelekea kwenye mikutano mikubwa ya
kampeni. |
MGOMBEA mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan
amevunja ngome ya chama cha ACT Wazalendo Mkoani Tanga pamoja na kuvuna
wanachama 272 kutoka vyama mbalimbali vya upinzani baada ya wanachama wa
vyama hivyo kujiunga rasmi na CCM.
Bi. Samia Suluhu ambaye ni mgombea mwenza wa Dk. John Pombe Magufuli
amefanikiwa kuvunja ngome za wapinzani leo mjini Tanga katika mikutano yake
ya kampeni baada ya wagombea udiwani watano wa ACT Wazalendo kujiunga na
CCM pamoja na wanachama wengine 235 toka Tanga mjini kujiunga na CCM kwenye
mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Usagara mkoani
Tanga.
Akihutubia katika mkutano mkubwa wa kampeni kunadi ilani ya CCM Tanga mjini
uwanja wa Usagara, Bi. Samia Suluhu aliwapokea wagombea udiwani watano
kutoka ACT Wazalendo, wakiwemo Wilson Elia (wa Kata ya Duga), Gasper Maboko
(Kata ya Nguvumali), Charles Luanda (Maweni) na Marry Scoty (Kata ya Tanga
Sisi) pamoja na Sada Mbwambo (viti maalum).
Mbali na madiwani hao kukihama chama cha ACT, wanachama 235 kutoka ACT, CUF
na Chadema walijiunga na CCM kwenye mkutano huo wa Tanga mjini huku wengine
37 wakijiunga na CCM katika mkutano mwingine ulofanyika Jimbo la Muheza
hivyo kutimiza wanachama 272 wapya kujiunga katika mikutano ya siku
hiyo.
Akizungumza na wanaCCM na wananchi waliojitokeza mkutano wa Tanga Mjini,
Bi. Suluhu aliwaomba kuichagua CCM kurudi madarakani ili kuendeleza
maendeleo iliyofikia katika maeneo mbalimbali, ikiwemo huduma za kijamii na
miundombinu hasa ya barabara. Alisema wapinzani hawafai kupewa madaraka kwa
kuwa hawajajipanga kimfumo kwani hata viongozi wanaogombea wamekimbia vyama
vyao na wanachotaka ni maslahi yao zaidi.
Alisema kwa mkoa wa Tanga Serikali ya CCM imepanga kuyakagua mashamba
makubwa yaliotwaliwa na wawekezaji na kutelekezwa kisha kuyarejesha kwa
wananchi ili waweze kuyatumia kwa uzalishaji, ikiwa ni pamoja na kupanua
bandari ya mkoa huo kuchochea maendeleo.
Aidha aliongeza kuwa wakulima wa zao la korosho hawana budi kuongeza
uzalishaji na kutokata tamaa kwani tayari Serikali inafanya mazungumzo na
Serikali ya Norway kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha kubangua korosho
mkoani hapo ili kuongeza thamani ya zao hilo. Alisema lengo la Serikali ni
kuhakikisha asilimia 40 ya vijana wanapata ajira kwenye viwanda vitakavyo
jengwa maeneo anuai ya nchi.
Bi. Samia alifanya mikutano minne mikubwa katika majimbo ya Mkinga,
Pangani, Mheza na Tanga Mjini na mikutano midogo midongo sita alioifanya
njiani akisimamishwa na wananchi wakitaka kumsikia alipokuwa akipita. Hata
hivyo katika mkutano wake wa Tanga Mjini baadhi ya wananchi walizidiwa
kutokana na msongamano na idadi kubwa ya watu na kuzimia kabla ya kupewa
huduma ya kwanza.
|
Gari ya Bi. Samia
Suluhu ikitoka kwenye kivuko cha Mv. Pangani II mara baada ya kuvushwa,
mgombea huyo mwenza wa urais CCM alikuwa akitoka kwenye mkutano wa hadhara
JImbo la Pambani leo. |
|
Kutoka kushoto ni
mgombea ubunge Jimbo la Pangani, Jumaa Hamid Aweso, Mwenyekiti wa CCM
Wilaya ya Pangani, Hamis Mnegero na Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu
Hassan wakizungumza jambo. |
|
Aliyekuwa mbunge wa
Jimbo la Nkenge, Asumpta Mshama akizungumza na wanaCCM na wananchi kwenye
mikutano ya hadhara leo katika baadhi ya Majimbo ya Mkoa wa Tanga. |
|
Moja ya ahadi za CCM
msimu wa Rais Jakaya Kikwete ikiendelea na ujenzi wa gati Wilayani Pangani
ikiendelea na ujenzi |
|
Bi. Samia Suluhu
akishuka ndani ya kivuko mara baada ya mkutano wa kampeni uliofanyika
Kijiji cha Mwera Jimbo la Pangani. |
|
Bi. Samia Suluhu
akihutubia mkutano wa kampeni Muheza. |
|
Baadhi ya wanachama
wapya waliojiunga na CCM wakiwa katika msitari mara baada ya kurejesha
fomu. |
|
Sehemu ya wanaCCM na wananchi ikiwa
imemsimamisha barabarani mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu
kumsikiliza alipokuwa njiani kuelekea kwenye mikutano mikubwa ya
kampeni. |
|
Sehemu ya wanaCCM na wananchi ikiwa
imemsimamisha barabarani mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu
kumsikiliza alipokuwa njiani kuelekea kwenye mikutano mikubwa ya
kampeni. |
|
Bi. Samia Suluhu
akiwa na mgombea ubunge wa Jimbo la Tanga Mjini Omary
Nundu(kulia). |
|
Mmoja wa wananchi
wakipewa huduma ya kwanza mara baada ya kuzimia kutokana na msongamano
katika mkutano wa kampeni kwa mbaya. |
|
Mkutano wa kampeni
wa mgombea mwenza Tanga Mjini leo. |
|
Mgombea Ubunge wa
CCM, Jimbo la Bumbuli, January Makamba akizungumza na wanaCCM na wananchi
katika mkutano wa kampeni. |
|
Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumpta
Mshama akizungumza na wanaCCM na wananchi kwenye mikutano ya hadhara leo
katika baadhi ya Majimbo ya Mkoa wa Tanga. |
|
Mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza Tanga Mjini
leo. |
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia