|
Eng.Philbert Rweyemamu akifafanua jambo katika moja ya mabanda ya
maonyesho kwa baadhi ya maafisa wa uhamiaji walipokuwa wakitembelea mabanda
ya maonyesho. |
|
Eng.Philbert Rweyemamu akifafanua jambo katika moja ya mabanda ya
maonyesho. |
|
Wageni wakijionea namna mradi wa matofali ya gharama nafuu
ulivyowanufaisha wenyeji wanaozunguka mgodi wa
Buzwagi. |
|
Wageni wakipata maelezo kutoka kwa wataalamu wa kampuni ya KALTIRE
ambayo imekuwa ikihudumia mgodi wa Buzwagi kwa kuwauzia matairi kwa ajili
ya mitambo ya uchimbaji mgodini hapo. |
|
Wageni pamoja na baadhi ya maafisa wa mgodi wa Buzwagi na wale wa
serikalini wakijionea matairi makubwa yanayotumika katika mgodi
huo. |
|
Wageni wakipata maelezo wakati walipotembelea banda la
PANAF |
|
Sehemu ya familia za wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi wakiwa
wameketi baada ya kutembelea mabanda mbalimbali |
|
Kama
vile hawaamini!!!! Ni kweli anacheza na nyoka hivyo? |
|
Kuhakikisha kumbukumbu hii haipotei kamera za simu zikafanya kazi
yake |
|
Kikundi hiki cha Ngoma kutoka Shinyanga kilitia fola kwa burudani
safi ya Ngoma waliyoitoa. |
|
Baadhi ya maafisa wakuu wa kampuni ya Acacia wakifuatilia burudani
ya ngoma |
|
Michel Ash-Afisa Mkuu wa Masuala ya uendeshaji wa kampuni ya Acacia
akizungumza na familia pamoja na wafanyakazi wa mgodi wa
Buzwagi |
|
Baadhi ya maafisa wa idara ya ufanisi wa Mgodi wa Buzwagi wakiwa
katika picha ya pamoja katika banda lao wakati wa
maonyesho |
|
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi mwenye shati la bluu akiongozwa na
mkuu wa kitengo cha ulinzi Jamal Rwambol kutembelea mabanda ya
maonyesho |
|
Azael
Kitange-Mkufunzi wa idara ya ufanisi wa kampuni akitoa maelezo kwa wageni
walipotembelea banda la idara ya Ufanisi katika kitengo cha
Mafunzo. |
|
Ufugali wa nyuki wa kisasa ni moja kati ya shughuli zinazofanywa na
mgodi wa Buzwagi kupitia idara ya Mahusiano ya Jamii kwa kuwawezesha
wenyeji wanaozunguka maeneo ya mgodi kujipatia shughuli zinazowaongezea
kipato. |
|
Wataalamu wa idara ya afya wakionyesha baadhi ya vifaa mbalimbali
vinavyotumika kupima afya za wafanyakazi wakati wote ili kuhakikisha afya
za wafanyakazi wa mgodi huo muda wote zinakuwa
salama. |
|
Wataalamu wa miamba wakionyesha aina mbalimbali za miamba yenye
dhahabu na namna wanavyotumia vifaa vya kisasa kuitafuta
dhahabu. |
|
Kikundi cha Ngoma cha kabila la wasukuma kikitoa burudani ya ngoma
wakati wa maadhimisho ya siku ya familia kwa wafanyakazi wa mgodi wa
Buzwagi |
|
Baadhi ya wanafamilia wa wafanyakazi wa mgodi wa
Buzwagi. |
Baadhi ya maafisa kutoka Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu wakifurahia
moja ya burudani wakati wa sherehe hizo.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Eng. Philbert Rweyemamu (katikati)
na Meneja wa Biashara wa Mgodi huo wakifuatilia kwa makini burudani
zilizokuwa zikiendelea wakati wa sherehe hizo, kushoto kwao ni mwakilishi
wa Mkuu wa wilaya ya Kahama.
Meneja Ufanisi wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Saimon Sanga akizungumza
na wafanyakazi wa Mgodi huo wakati alipokuwa akimkaribisha meneja Mkuu wa
mgodi wa Buzwagi.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Eng.Philbert Rweyemamu akizungumza
na wafanyakazi wa Mgodi huo pamoja na familia zao wakati wa sherehe za siku
ya familia.
Watoto wakishiriki michezo mbalimbali iliyokuwepo maalum kwa ajili
yao
Watoto wakishiriki michezo wakati wa sherehe
hizo.
Graham Crew-Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu (kushoto) akiteta
jambo na Michelle Ash-Afisa Mkuu wa masuala ya uendeshaji wa kampuni ya
Acacia wakati wa sherehe hiyo
Mtaalamu wa masuala ya uchimbaji wa Mgodi wa Buzwagi akitoa maelezo
kwa wageni waliotembelea banda la idara yake.
Mmoja
wa wafanyakazi wa wa Idara ya masuala ya usalama wa Mgodi wa Buzwagi akitoa
maelezo kwa baadhi ya familia za watumishi wa mgodi huo wakati walipo
tembelea banda maalum la maonyesho la idara ya usalama
mgodini.
Mmoja
wa wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi Bwana Moses Msofe akiwa na familia yake
kusherekea siku ya familia
Wazazi wakiwasimamia watoto wao walipokuwa wakishiriki michezo
mbalimbali ya watoto.
Watoto wa baadhi ya wafanyakazi wa Mgodi huo wakifurahia michezo
mbalimbali wakati walipokuwa wakiadhimisha siku ya familia mgodini
hapo
Baadhi ya ndugu wa wafanyakazi wa Mgodi wa Buzwagi wakiangalia aina
mbalimbali za mashine zinazotumika katika shughuli za uchimbaji katika
mgodi huo.
Moja
kati ya magari makubwa kabisa yanayotumika katika mgodi huo likiwa katika
eneo la maonyesho.
Kutoka kushoto ni meneja wa uendelezaji wa Mgodi wa Buzwagi George
Mkanda, katikati ni Graham Crew-Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu na
Michelle Ash-Afisa Mkuu wa masuala ya uendeshaji wa kampuni ya Acacia
wakati wa sherehe za siku ya familia ya Mgodi wa
Buzwagi.
|
Baadhi ya familia za watumishi wa Mgodi wa Buzwagi zikitambulishwa
wakati wa hafla hiyo. |
Buzwagi imeanzisha mkakati wa kukuza na kuboresha hali ya utendaji
kazi kwa wafanyakazi wake kwa kuanzisha utaratibu wa kuwakutanisha
wafanyakazi wa mgodi huo na familia zao mara moja kwa mwaka katika siku
maalumu ya familia ambayo hutoa fursa kwa familia za wafanyakazi wa mgodi
huo kuweza kujionea namna ambavyo shughuli za uchimbaji wa madini hufanyika
na hivyo kuwa mabalozi wazuri wa kampuni kwa
ujumla.
Mwaka huu wafanyakazi wa kampuni hiyo wamepata fursa ya kukutana na
kujionea shughuli mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanyika mgodi hapo. Pamoja
na mambo mengine wafanyakazi hao pia walipata fursa ya kutembelea eneo
ambapo shughuli za uchimbaji zinafanyika.
Sherehe hizo zilihudhuliwa na Afisa mkuu wa masuala ya
uendeshaji Michelle Ash, Meneja Mkuu wa Mgodi wa
Bulyanhulur-Graham Crew na meneja mkuu wa masuala ya ufanisi wa
kampuni Janet Ruben pamoja na meneja mahusiano na mawasiliano wa Acacia
Nector Foya, pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali..