Umati wa wanaCCM na
wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa Mnazi Mmoja nje
kidogo ya mji wa Lindi Mjini kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa
Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu.
|
Umati wa wanaCCM na
wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa Mnazi Mmoja nje
kidogo ya mji wa Lindi Mjini kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa
Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu. |
|
Umati wa wanaCCM na
wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa Mnazi Mmoja nje
kidogo ya mji wa Lindi Mjini kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa
Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu. |
|
Mke wa Rais Kikwete,
Mama Salma Kikwete akizungumza na umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama
hicho uliokuwa umefurika katika uwanja wa Mnazi Mmoja nje kidogo ya mji wa
Lindi Mjini kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha
Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu. |
|
Katibu, Itikadi na
Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na wanaCCM na wananchi kwenye
mkutano wa kampeni za mgombea mwenza wa CCM, Mama Samia Suluhu jana Mkoani
Lindi. |
|
Bi. Samia Suluhu
(kulia) akimtambulisha mgombea mmoja wa wagombea udiwani katika Jimbo la
Mchinga, kuzungumza na wapiga kura wa eneo hilo. |
|
Samia Suluhu akimpokea mmoja wa wanachama mpya
aliyejiunga na CCM katika Jimbo la Mchinga. |
|
Bi. Samia Suluhu
akimpokea mmoja wa wanachama mpya aliyejiunga na CCM katika Jimbo la
Mchinga. |
|
Mmoja wa wanachama
wapya wa CCM aliyejiunga na CCM mara baada ya mkutano wa kampeni wa mgombea
mwenza katika Jimbo la Mchinga. |
KAMPENI za mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu zinazoendelea mkoani Lindi zimekuwa
tishio kwa vyama vya upinzani baada ya mkutano uliofanyika jana eneo la
Mnazi Mmoja nje kidogo ya mji wa Lindi Mjini kuzoa wanachama 61 waliotoka
upinzania na kujiunga na CCM.
Mkutano huo wa kampeni uliohudhuriwa pia na Mke wa Rais Mama Salima Kikwete
umeacha maumivu kwa vyama vya upinzani vya CUF, Chadema na NCCR-Mageuzi
baada ya kujikuta wanachama 61 wakivikimbia vyama vyao na kujikuta
wakijiunga na Chama Cha Mapinduzi na kukabidhiwa kadi mpya za CCM kila
mmoja.
Miongoni mwa wanachama ambao walipokelewa leo ni pamoja na Katibu wa
Chadema Wilaya ya Lindi Mjini, Abdullah Madebe, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi
Mtaa wa Nananji Lindi, Bakari Kalulu na wanachama wengine kutoka vyama vya
CUF na Chadema. Akizungumza baada ya kumkabidhi kadi, Bi. Samia Suluhu
Katibu wa Chadema Wilaya ya Lindi Mjini alisema awali alipokuwa upinzani
alikuwa amepotea na amegunduwa kuwa alikuwa anapoteza muda hivyo kuomba
wananchi wamsamehe na ameamua kurudi kundini na kuendelea kulkijenga
taifa.
Akizungumza baada ya kuwapokea wanachama hao, mgombea mwenza Suluhu alisema
Serikali ya awamu ya tano imeandaa mambo mengi mazuri kwa mikoa ya Lindi na
Mtwara na jambo la kwanza kulifanya baada ya kuunda serikali ni kuubadili
mji wa Mtwara na Lindi kuwa miji ya viwanda, hali ambalo itakuza uchumi kwa
kiasi kikubwa hivyo kunufaisa wananchi.
Alisema kwa kuanzia Serikali inajenga viwanda vinane mkoani Mtwara na
vingine vitajengwa mkoani Lindi viwanda ambavyo vitategemea gesi katika
uzalishaji wake bidhaa ambayo tayari inapatikana kwa wingi katika maeneo
hayo. Alisema ujenzi wa viwanda utaongeza kasi ya ukuaji wa uchumi na
kuongeza nafasi za ajira jambo ambalo litawanufaisha wakazi wa eneo hilo na
wawekezaji.
"...Tunataka kuitenga Lindi kuwa mji wa viwanda vitakavyoitumia gesi kwa
uendeshaji, lengo ni kuwa na viwanda vitakavyozalisha nafasi za ajira
takribani asailimia 40...," alisema Bi. Suluhu. Awali akihutubiwa katika
mkutano wa kampeni ulofanyika Kata ya Mingumbi Kilwa Kusini, alisema
Serikali inatambua hali ya kuyumba kwa soko la korosho na ufuta ili
kukabiliana na hali hiyo imejipanga kujenga viwanda vya kubangua na kufunga
korosho pamoja na kukamua mafuta kwa lengo la kumuongezea thamani mkulima
katika zao analozalisha.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa Mnazi Mmoja Katibu, Itikadi na
Uenezi wa CCM, Nape Nnauye aliwatoa hofu akinamama na wapiga kura wengine
juu ya vitisho vya kuwepo na vurugu kipindi cha uchaguzi kwa lengo la
kuwatisha wapiga kura, hivyo kuwataka wananchi wasiogope kwani Serikali na
CCM kupitia vijana wake imejipanga kupambana na wafanya fujo hao.
Alisema kitendo cha kutoa vitisho kwa wapiga kura ni kuibaka demokrasia
hivyo CCM na vijana wake hawatakuwa tayari kuona demokrasia inabakwa nchini
na wapuuzi wachahe. "...Vijana wa CCM naomba mkikamata kibaka wa demokrasia
shughulikeni naye kidogo kabla ya kumpeleka polisi...CCM itashinda kwa
kishindo," alisema Nape Nnauye.
Aidha msemaji huyo wa Chama Cha Mapinduzi alisema mgombea urais wa Chadema,
Edward Lowassa pamoja na mpambe wake anayemuunga mkono Fredrick Sumaye
hawawezi kuiponda Serikali ya CCM kwa kuwa wao wamekuwemo na kushika nafasi
za juu za utendaji ndani ya serikali na kama walishindwa kuleta mabadiliko
hawawezi kufanya hivyo leo.
Aliongeza kuwa kitendo cha kuendelea kuiponda ni sawa na kujidhalilisha wao
wenyewe kwa wananchi hivyo kuwataka wasiwarubuni Watanzania kwamba
wanamabadiliko ya msingi zaidi ya maslahi yao binafsi, ambayo ndiyo
yanayowasukuma kukimbilia walipo.
Mgombea mwenza wa urais CCM, Bi. Suluhu bado anaendelea na ziara ya kuinadi
ilani ya Chama Cha Mapinduzi Mkoani Lindi na baada ya kumaliza majimbo ya
mkoa huo ataendelea katika Mkoa wa Mtwara, kuwashawishi wananchi kuichangua
CCM ili iweze kupata ridhaa ya kuunda Serikali ya awamu ya tano.
|
Baadhi ya wanaCCM na
wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Bi.
Suluhu kwenye Jimbo la |
|
Kutoka kushoto ni
mgombea mwenza wa CCM nafasi ya uraisa, Bi. Samia Suluhu na Mkuu wa Mkoa wa
Lindi, Mwantumu Maiza na mgombea wa Jimbo la Mchinga Said Mtanda wakiwa
kwenye mkutano wa kampeni katika Jimbo la Mchinga jana. |
|
Mgombea Jimbo la
Mchinga Said Mtanda akizungumza na wannaCCM na wananchi jana jimboni kwake
ambapo mgombea mwenza alihutubia wananchi. |
|
Sehemu ya wanaCCM na wananchi jana jimboni kwake
ambapo mgombea mwenza alihutubia wananchi. |
|
Mbunge wa Afrika
Mashariki na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam, Anjela Kiziga
akizungumza katika mkutano wa kampeni za CCM. |
|
Aliyekuwa Mjumbe wa
Kamati ya Ushindi Chadema Taifa, Greison Nyakarungu ambaye kwa sasa
amejiunga na CCM akizungumza katika moja ya mikutano ya kampeni ya
CCM. |
|
Aliyekuwa Mbunge wa
Jimbo la Nkenge, Asumpta Mshama akipiga madongo kwa wapinzani kwenye moja
ya mikutano ya kampeni ya CCM. |
|
Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa
umefurika katika uwanja wa Mnazi Mmoja nje kidogo ya mji wa Lindi Mjini
kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi, Bi.
Samia Suluhu. |
|
Katibu, Itikadi na
Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Lindi,
Bi. Mwantumu Mahiza. |
|
Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa
umefurika katika uwanja wa Mnazi Mmoja nje kidogo ya mji wa Lindi Mjini
kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi, Bi.
Samia Suluhu. |
|
Mkuu wa Mkoa wa
Lindi, Mwantumu Mahiza akizungumza na wanaCCM na wananchi kwenye mkutano wa
kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Mama Samia Suluhu. |
|
Mke wa Rais Kikwete,
Mama Salma Kikwete, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi, Mzee Ally Mtopa pamoja
na mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu wakijadiliana
jambo kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM viwanja vya Mnazi
Mmoja. |
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia