Aliyekuwa
Katibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa Frank Leonard
(Kulia) akifungua mkutano mkuu wa IPC jana katika ukumbi wa Maktaba ya
Iringa katikati ni Daud Mwangosi ambaye alikuwa ni mwenyekiti wa IPC
akifikiri jambo.
Aliyekuwa mwenyekiti wa IPC Daud Mwangosi (kushoto) akihojiwa na
mzee wa matukio daima Bw Francis Godwin ambaye alikuwa ni katibu
msaidizi wa IPC juu ya wanahabari kudumisha umoja na mshikamano wakati
wa uhai wake.
Mwandishi
wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa cha chama cha
waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi tarehe Kama ya leo
miaka mitatu iliyopita aliuwawa katika vurugu za Polisi na wafuasi wa
Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa .
Mwanahabari
huyo Daud Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za
Chadema Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi .
Kabla
ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yaliweza kupigwa eneo hilo
kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika
eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa haapo tayari kuondoka katika ofisi
yao.
Chanzo
cha mwanahabari Mwangosi kuuwawa kilitokana na kukamatwa kwa mwandishi
wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa Godfrey Mushi na hivyo
mwanahabari huyo kkutaka kuhoji polisi sababu ya kukamatwa kwa
mwanahabari huyo ndipo askari hao walipoanza kumshambulia kwa kichapo na
baadae mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo na mwandishi huyo na
askari mmoja waliaguka chini .
Ndani
ya dakika tano ilisikika sauti kutoka kwa askari huyo kuwa afande
nimekufa ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya ya Mufindi
huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti .
Katika
vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa
Chadema kurushiana mawe kwa mabomu zaidi ya magari matano ya Chadema na
ya wananchi yameharibiwa huku watu kadhaa wamejeruhiwa na mwanahabari
mmoja Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya.
Hii ni taarifa ya Jeshi la polisi kabla ya tukio kwa vyombo vya habari
JESHI
la polisi mkoa wa Iringa limesema limezuia mikutano ya vyama vya siasa
kwa vyama vyote na sio kwa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA)
pekee hivyo laonya vyama vyote kutii sheria bila shuruti.
Hata
hivyo jeshi hilo la Polisi limesema kuwa halifanyi kazi kwa matakwa ya
chama chochote cha siasa na kuwa si kweli kama wanavyodai viongozi wa
Chadema kuwa jeshi la polisi linatumiwa na chama cha mapinduzi (CCM)
kuzuia mikutano hiyo.
Kamanda
wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamuanda ametoa kauli hiyo leo
ofisini kwake alipozungumza na waandisha wa habari kuhusu zuio la
mkutano wa Chadema uliopangwa kuanza leo katika wilaya ya Mufindi.
”
Nawatangazia wanasiasa na vyama vyote vya siasa pamoja na wananchi wa
mkoa wa Iringa kuwa hakutakuwa na mikutano ya kisiasa kutokana na
shughuli za sensa zinazoendelea ….hivyo basi nawaomba wananchi wote
kutoshiriki mikutano yoyote ya kisiasa itakayoitishwa na wanasiasa
“alisisitiza
Kuwa
mikutano hiyo imezuiliwa kwa kipindi hiki cha sensa kilichoongezwa hadi
hapo tamko litakapotolewa tena na msajili wa vyama vya siasa John
Tendwa kama alivyokwisha kutoa tamko la kuzuia shughuli hizo za vyama
vya siasa kwa kipindi hiki cha sensa.
“Wananchi
wote wa mkoa wa Iringa mnaombwa kutii sheria bila shuruti hii ni amri
….nawaombeni sana wananchi kutodanganywa na wanasiasa kwa kuvunja sheria
“aliongeza kamanda huyo wa polisi.
Hata
hivyo alisema kuwa kimsingi zoezi la sensa lilipaswa kuhitimishwa
Septemba mosi mwaka huu ila kutokana na serikali kuongeza muda wa zoezi
hilo bado jeshi hilo la polisi linazingatia maagizo ya Msajili wa vyama
vya siasa kama alivyoyatoa kwa jeshi hilo.
Kamanda
Kamuanda alisema kuwa jeshi hilo la polisi wala msajili wa vyama vya
siasa hajazuia vyama vya siasa kuendelea na vikao vyao vya ndani kwa
kipindi hiki na kuwa hata Chadema wakiwa mkoani Iringa wameendelea
kufanya vikao vyao vya ndani katika kata mbali mbali za mkoa wa Iringa
na hakuna mtu aliyewazuia kuendelea kufanya hivyo.
Majibu ya Dkt Slaa
Wakati
jeshi la polisi likipinga shughuli hizo za vyama vya siasa kufanya
mikutano ya hadhara katibu mkuu wa Chadema Taifa Dkt Willbroad Slaa
ameibuka na kusema kuwa chama chake kitaendelea na mikutano kama
kilivyojipangia na kuwa wapo tayari kwa lolote litakalojitokeza .
Dkt
Slaa alisema kuwa walivumilia mara ya kwanza walipozuiwa mikutano hiyo
mkoani Iringa na kuvuta subira hadi jumamosi zoezi hilo lilipomalizika
sasa anashangazwa kuona jeshi hilo likiendelea kuzuia mikutano hiyo
tena.
“Tumemsikiliza
kamishina wa sensa Hajati Amina Mrisho Said kuwa hadi sasa watu
asilimia 95 wameandikishwa huku akiwata wale ambao bado kuwapigia simu
wenyeviti wa mitaaa na vijiji ili wakaandikishwe na makarani wa sensa
….sasa jeshi la polisi linataka kutuambia kuwa hao watu asilimia 5
waliobaki wapo Iringa peke yake hadi wakazuia mikutano yetu? tunasema
hatutakubali tutaendelea na mikutano yetu kama kawaida hatupotayari
kabisa kusubiri hadi tarehe nane” alisema Dkt Slaa.
Pia
alisema kuwa kama ni uzalendo sasa umefika kikomo na kuwa wataendelea
na ratiba zao za mikutano kama ilivyopangwa na watapambana kwa lolote .