MTOTO HAPPY LIMWAMWA (9-10) AKIMBIA KIPIGO ALIPOKUWA AKIFANYA KAZI ZA NDANI NJOMBE

  Happy  Limwamwa (9-10) Pichani
   Happy  Limwamwa 9-10 (kushoto) akizungumza kwa uchungu  kwa Msaidizi wa Kisheria Geophrey Kaduma, (wapili kulia)  manyanyaso aliyokuwa akiyapata toka kwa mama aliyekuwa amemtowa kwao Wilaya ya  Mbinga Mkoa wa Ruvuma, kwa malengo ya kufanya kazi za ndani, ndipo alipokutana na kichapo toka kwa mama huyo na mume wake na kumfanya akimbiye na kuishi mitaani na kuokotwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bryceson Mgaya wa Mtaa wa Kambarage Kata ya Njombe Mjini  Wilaya  ya Njombe Mkoa wa Njombe, Pamoja na Mwenyekiti huyo kutowa taarifa katika kituo cha Polisi na kumtembeza katika mitaa tofauti alipokuwa akifanya kazi  zaidi ya wiki 3  bado juhudi yoyote haijazaa matunda kwa  mtoto huyo kurudishwa kwao, kwa yoyote anaye weza kumfaham mtoto huyo awasiliane na Mwenyekiti huyo wa Mtaa, 0766336403, Mwenyekiti wa Kituo cha Sheria Geophrey Kaduma, 0759601915-o655601915. wapili kushoto ni Katibu wa Kituo cha Msaidizi wa Kisheria Magy Mtalla na wakwanza kulia ni mke wa mwenyekiti wa Mtaa wa Kambarage Matha Maiseli (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
 Katibu wa Kituo cha Msaidizi wa Kisheria Magy Mtalla, akizungumza na mtoto huyo Happy  Limwamwa 9-10
Happy  Limwamwa 9-10 akiwa katika picha

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post