Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Mizengo Pinda akiwa anakata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua magari ya kubeba wagonjwa ambayo ameyakabidhi leo mkoani Arusha kwa ajili ya kupelekwa wilayani Ngorongoro kwa ajili ya kutumika kwa ajili ya kubeba wagonjwa
waziri pinda akiwasili katika jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha
Waziri mkuu akielekea kukabidhi rasmi magari mawili ya kubebea wagonjwa
mkuu wa mkoa wa Arusha akiongeozana na waziri mkuu kwa ajili ya makabidhiano ya magari ya kubebea wagonjwa yaliyoletwa na waziri
habari picha na Woinde Shizza,Arusha
Waziri mkuu wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda leo amekabithi magari mawili ya kubebea wagonjwa yenye dhamani ya shilingi milioni 150.
Magari hayo ambayo yamekabidhiwa, yametokana na ahadi ambayo waziri huyo alitoa Kwa Wananchi wa wilaya ya ngorongoro wakati Alipofanya ziara wilaya ni humo september 2013.
Akizungumza wakati akikabidhi magari hayo waziri mkuu Mizengo Pinda alisema wakati alipokuwa kwenye ziara wilaya ni humo, alipokea malalamiko ya kutakuwepo na magari ya kubebea wagonjwa hali ambayo ili mfanya atoe ahadi nasasa ameamua kuitekeleza.
"nilipata malalamiko nikapeleka wizara ya afya, wakapokea na kaniambia watafanyia kazi sasa Kila nikiwauliza Wakaniambia bado sasa nikabahatika kupata safari ya Kwenda japani nilipoenda Nitakuja na na Wananchi wa Tanzania wa naishi uko nikawaomba wa nisaidie japo gari moja ya kubebea wagonjwa sasa wao ndio wakaja wakanipa magari haya mawili "alisema pinda
Alisema Kuwa mara baada ya kupokea magari hayo aliyafanyia ukarabati mdogo na sasa ameamua kuyaleta Mkoani ili yapelekwe katika wilaya husika ambapo alisema Kuwa mara baada ya kufikishwa wilaya ni ngorongoro gari moja litatumika katika hospitali ya waso huku ingene ikitumika hospitali ya Enduleni.
Aidha aliwataka viongozi wa wilaya ya ngorongoro kutumia vyema magari hayo haswa katika shughuli iliolegwa, Pamoja na kuyatunza ili ya weze kutumika na kubeba wagonjwa wakati Mgonjwa anapotokea au tatizo la gafula linapotokea.
Aidha alibainisha Kuwa magari haya ameyatoa yeye mwenyewe kutoka Kwa wa fadhili na sio magari ya wizara hivyo wakapokee haya wakijua ni ahadi ya waziri mkuu, na sio ya wizara hivyo wapokee haya wakati wakiwa Wana ngoja magari ya kubebea wagonjwa kutoka wizarani
Alipokea msaada huo mkuu wa wilaya ya ngorongoro Ashimu Mgandila alisema Kuwa wa nashukuru sana Kwa msaada hii kwani Wananchi haswa wakina mama waja wa zito wali Kuwa wanateseka sana wakati walipo Kuwa wa naumwa.
Alisema Kuwa wali Kuwa na gari ya kubebea wagonjwa lakini imearibika Kwa kipindi karefu ila hii itakuwa ni suluisho Kwa Wananchi wa wilaya hiyo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya ngorongoro John kulwa alisema Kuwa magari haya ni ukumbozi hasa Kwa upande wa wamama Pamoja na wagonjwa mahututi kutaka katika Kila kata na Kila kaya.