Ticker

6/recent/ticker-posts

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA HANANG DERICK MAGOMA ASEMA KUWA CHADEMA HAWANA IMANI NA MSIMAMIZI WA UCHAGUZI JIMBO KWAKE

Mgombea Ubunge Jimbo la Hanang Derick Magoma akizungumza na waandishi wa

Habari (hawapo pichani) juu ya kutokua na imani na Msimamizi wa Uchaguzi wa
Jimbo hilo ambaye ni Mkurugenzi wa Wilaya ya Hanang Felix Mabula madai
ambayo wamewasilisha kwa tume ya uchaguzi iteue Msimamizi ili kufanikisha
uchaguzi huru na wa haki.Kushoto ni Mwenyekiti wa Chadema Hanan`g  Isack
Joseph  na kulia ni Mgombea udiwani kata ya Endasiwold John Farayo habari   Picha
na woinde shizza

Wagombea wa Nafasi za Ubunge na Udiwani katika Wilaya ya Hanang iliyoko

mkoa wa Manyara wamedai kutokua na imani na Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Hanang , Felix Mabula ambaye ni Msimamizi mkuu wa uchaguzi katika jimbo
hilo kwa madai kuwa Mkurugenzi huyo alikumbwa na tuhuma nyingi za matumizi
mabaya ya fedha kwenye miradi ya maji na kuboresha miundombinu ya shule za
msingi tuhuma ambazo ziliibuliwa na madiwani wa CHADEMA  ambao ni wagombea
kwa sasa jambo linalowapa wasiwasi kuwa haki haitatendeka katika uchaguzi.





Mgombea Ubunge katika jimbo la Hanang Derick Magoma alisema hayo wakati
akizungumza na Waandishi wa Habari ,amesema kuwa tayari wameandikia barua
tume ya Uchaguzi yenye kumbukumbu namba CDM/HAN/UT/2/239  juu ya kutokua na
imani na msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo barua waliyoiwasilisha
septemba 2 mwaka huu wakiitaka tume iteue Msimamizi mwingine.





Magoma alisema kuwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha zilijadiliwa katika
Baraza la Madiwani zikiongozwa na madiwani wa CHADEMA ambao ni Ndugu Peter
Lori Diwani wa Kata ya Katesh,John Farayo Diwani kata ya Endasiwold ,Masala
Bajuta wa kata ya Gisambalang na wengine wengi.





“Madiwani hao waliomtuhumu Mabula  ndio wagombea    na hao hao Mabula
atasimamia uchaguzi wao ,tunaona kabisa kuwa haki haiwezi kutendeka ,na
hata kama ikitendeka hatutaamini kama imetendeka” Alisema Magoma





Mgombea huyo alisema kuwa Mabula anakabiliwa na tuhuma za kutumia vibaya
shilingi bilioni 1 na milioni 100 ambazo zimepotea na zingetumika kujenga
vituo vya afya ,kuleta madawa na kusambaza huduma ya maji safi ambayo ni
changamoto kubwa kwa jimbo hilo.





Mgombea udiwani kata ya Endasiwold John Farayo alisema kuwa wao kama
wagombea hawana imani na Mkurugenzi huyo hivyo wameitaka tume ya uchaguzi
ichukue hatua za haraka kumteua msimamizi mwingine wa uchaguzi ili uchaguzi
uwe huru na wa haki.





Mwenyekiti wa Chadema Hanan`g  Isack Joseph alisema kuwa chama hicho
kimesimamisha wagombea  udiwani 31 kati ya kata 33 na kufafanua kuwa
kutokana na rekodi ya Mkurugenzi huyo wanahitaji msimamizi mwingine wa
uchaguzi ambaye watakua na imani naye.

Post a Comment

0 Comments