Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwasili kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Matarawe, Songea Mjini, Mkoani Ruvuma leo Septemba 1, 2015, ambako kumefanyika Mkutano wa Kampeni zake anazoendelea nazo kwa nchi nzima. Mh. Lowassa amepata mapokezi makubwa sana mkoani hapo, akitokea Mkoa wa Njombe.