Na Woinde Shizza,Arusha
Baada
ya kutokuwepo kwa mbio za riadha zijulikanazo kama mount meru Marathon kwa
miaka 15 sasa ,hatimaye wadau wa mchezo wamjitokeza na kurudisha mbio hizo
ambazo zinatarajiwa kufanyika octoba 4 jijini Arusha.
Mbio hizo za km 21 zilifanyika mara ya mwisho mwaka 2000,ambapo
hazikuendelea tena kutokana na kukosa wadhamini hali iliyopelekea kukosa hamasa
kwa wanariadha mabalimbali.
Katibu wa chama cha riadha mkoani hapa Alfredo Shahanga
alisema kwuwa mbio hizo ni za wazi na zitashirikisha wanariadha wanawake na
wanaume mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kwa
wanariadha ambao watakuwa tayari kuja kushiriki.
“Mashindano haya chimbuko lake ni mkoani hapa na mara ya mwisho kufanyika ilikuwa ni mwaka 2000 kipindi hicho yakiitwa ‘Mount meru International Marathon’ yalishindwa kuendelea kufanyika kutokana na kuwa wale waandaaji wa miaka hiyo walifikia mahali mahali wakasitisha kutokana na sababu za kifedha”alieleza Shahanga.
Mbio hizo zinaandaliwa na Mambo jambo digital centre kwa kushirikiana na
chama cha riadha mkoani hapa zitaanzia mnara wa
saa zitazunguka kuelekea barabra ya sokoine mpaka uwanja wa ndege
baadae zitamalizikia uwanja wa mpira wa sheikh Amri Abeid.
Shahanga ambaye pia ni katibu wa Chama cha Riadha