-->
|
Baadhi ya wasanii wakimsikiliza Salma Moshi |
Jukwaa La Sanaa la BASATA wiki hii lilipata wazungumzaji wa
aina yake na kulifanya kuwa jukwaa lililochangamka na kuwa na mazungumzo ya
zaidi ya masaa matano. Wasanii takriban 70 walikaa wakichambua maada mbalimbali
kuhusu mustakhabari wa sanaa katika nchi yetu. Jambo ambalo liliingiza
changamoto katika jukwaa hili, ni kuweko katika meza kuu wasanii wawili ambao
walianza sanaa nchini na hatimae kuhamia ughaibuni ambako ndiko wanaishi kwa
sasa.
Wasanii
Salma Moshi aliyekuwa akijulikana kama Salma Nyoka,
msanii wa kwanza wa kike kuchezea nyoka katika jukwaa, na ambaye alikuwa
kiongozi wa vikundi vilivyotamba kama DDC Kibisa Cultural Troupe Super
Mama Cultural Troupe na Ujamaa Cultural Troupe, na Abbu Omar,
mwanamuziki aliyewahi kupigia bendi kama Urafiki na UDA Jazz ambae
kwanza
alihamia Kenya na kupiga na kurekodi na makundi kama Simba wa Nyika na
Les
Wanyika na pia kurekodi album kadhaa akiwa na kundi lake ambaye hatimae
alihamia Japan ambako amekuwa akiishi kwa kupiga muziki na akiwa na
waTanzania
wengine kama Lista na Fresh Jumbe.
Mazungumzo
yaligusia nyanja mbalimbali ikiwemo umuhimu wa
kuwa na mikataba kabla ya kazi, kuboresha kazi ili kuweza kuuza nje,
namna ya kujitambulisha duniani kwa kuwa na websites na blogs, na pia
serikali kubadilika na kuweko
mfumo wa uongozi wa sanaa kuanzia ngazi ya wilaya hadi Taifa. Katika
mkutano
huo, John Kitime Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki aliongelea fursa ya
Bima
ya Afya kwa wasanii, ambapo Salma Moshi alijitolea kuwalipia nusu ya ada
wasanii wanne, na kumlipia bima kamili Mzee Kassim Mapili ambaye kwa
sasa
anasumbuliwa na moyo na figo. Abbu Omar pia aliamua kulipia Bima yake na
kueleza kuwa katika nchi ya Japan ni lazima kila mwananchi kuwa na Bima
ya Afya, kwani ugonjwa hauji kwa taarifa na matibabu ni gharama kubwa.
Mkutano huo ulianza saa tano na kulazimishwa kusimamishwa
saa kumi, kwani wasanii bado walikuwa na mengi ya kuwauliza wasanii hawa nguli
walioweza kuendeleza maisha ughaibuni kupitia sanaa
|
Mwandishi maarufu Khadija Khalili (mwenye daftari) akifuatilia maada |
|
Mwenyekiti wa CHAMRUMBA akiwa na Mzee Mapili |
|
Francis Kaswahili mwenye kofia Mwenyekiti TAFOMUDEA |
|
Abbu Omari mwanamuziki aishiye Japan |
|
Salma Moshi na Mzee Mapili |
|
Meza Kuu |
|
Group Picture |
|
Salma akiwa na baadhi ya wasanii aliowalipia sehemu ya Bima ya Afya
|
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia