MAAMUZI YA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KUHUSU RUFAA ZA WABUNGE


Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepokea jumla ya rufaa 54 za madiwanikupinga Maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi katika majimbo mbalimbali nchini. Pia jumla ya rufaa 198 za madiwani kutoka Halmashauri mbalimbali.
Tume imeanzakupitia vielelezo vilivyowasilishwa na Wagombea (warufani) na Wasimamizi wa Uchaguzi kutoka majimboni. Imeanza kuzitolewa maamuzi rufaa za Wabunge.  Leo tarehe 31/82015 zimejadiliwa na kuamuliwa rufaa 38. Zilizobaki mawasiliano yanaendelea kati ya Tume na Wasimamizi wa Uchaguzi ili kupata vielelezo vinavyohusika kuisaidia Tume kufikia maamuzi ya kisheria na haki kwa wagombea na vyama vyote vinavyoshiriki katika uchaguzi.  
Wagombea waliokuwa wamewekewa pingamizi na kuenguliwa na Wasimamizi wa Uchaguzi ni 16 na Tume imerudisha wagombea 13kati ya hao, waliobaki ni 3 ambao Tume imeridhia maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi. Hii ni kutokana na vielelezo vilivyowasilishwa kutoonesha makosa ya kisheria au kiufundi.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post