Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth John Magufuli
akiwasalimia wananchi wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua mumewe Dkt
John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika
awamu ya tano,kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa wa Oktoba 25 mwaka
huu.
Mara bada ya kuhutubia chumba chetu cha habari
kilihemewa na simu za wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kuelezea
furaha yao sio tu kwa kumuona jukwaani bali pia kwa kuongea kwa kujiamini.
Mama Magufuli amekuwa haonekani sana kwa sababu ya kuuguza mgonjwa nyumbani
kwao Chato. Wamesema wametiwa moyo sana na haiba ya Mama Magufuli na
wameshangazwa kwa uwezo wake mkubwa wa kuongea mbele za watu bila woga na
bila kumung'unya maneno.
Wananchi wa Chato wakimshangilia Mama Magufuli kwa
shangwe kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa
shule ya sekondari Chato mkoani Geita.