Kamati ya Miss Tanzania inapenda kuwatangazia wadau wote
wanaotaka kuandaa Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania kwa mwaka 2016 kutuma
maombi yao ya uwakala kuanzia sasa hadi tarehe 30 Novemba 2015 ndio mwisho wa
kupokea maombi ha yo.
Mashindano yatakayo fanyika ni ya mikoa tu, hakutakuwa na
mashindano katika ngazi ya kitongoji, wilaya wala Kanda.
Sifa za kuwa Wakala wa Miss Tanzania ni pamoja na
1)
Uwe na Kampuni iliyosajiliwa na Mamlaka husika ya Serikali.
2)
Uwe na mtaji wa kutosha.
3)
Uwe na uwezo wa kuandaa shindano katika ufanisi mkubwa.
4)
Uwe mstari wa mbele katika kukuza sanaa za utamaduni
nchini.
Wakala atakaye pitishwa na Kamati ya Miss Tanzania atapaswa
kujisajili Baraza la Sanaa la Taifa.(BASATA) kabla hajapewa kibali cha kuandaa
shindano.
Wilaya za Mkoa wa D’salaam, Ilala, Kinodoni na Temeke
zitapewa hadhi ya Kimkoa, ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Elimu ya Juu.
Ada ya Uwakala ni shilingi milioni moja(1,000,000/-).
Ada ya Uwakala italipwa kwa Kamati ya Miss Tanzania baada ya
maombi kukubaliwa na kupitishwa.
Maombi yatumwe kwa barue pepe misstanzania2015@yahoo.com
Kwa mawasiliano na ufafanuzi zaidi piga namba zifuatazo:-
0673 521037 Katibu wa
Kamati
0754 337043 Msemaji wa Kamati
0755 019288 Sekretariet.
Imetolewa na:
JUMA PINTO.
MWENYEKITI
KAMATI YA MISS TANZANIA.