Raisi Jakaya
Kikwete amewataka viongozi wa nchi za Afrika kuipa nguvu mahakama ya Afrika ya
Haki za binadamu iliyoko jijini Arusha ili iweze kusikiliza za kesi za jinai badala ya kupelekwa moja kwa moja kwenye
mahakama ya kimatifa ya makosa ya jinai.
Kikwete
amesema kuwa iwapo Mahakama hiyo itapewa
nguvu itarahisisha upatikanaji wa haki za raia katika bara la Afrika na
kuimarisha misingi ya utawala bora na kuheshimu haki za Binadamu.
Akihutubia
Mahakama hiyo jana Raisi Kikwete
alizindua kitabu chenye taarifa
muhimu za mahakama hiyo kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili ,amesema kuwa ni
hatua mojawapo katika kuhakikisha lugha hiyo inatumika mahakamani hapo na
kuwawezesha Watanzania wengi na Waafrika kuelewa shughuli za mahakama hiyo na
utendaji kazi wake.
Raisi wa
Mahakama hiyo Jaji Agustino Ramadhani amesema kuwa itachukua muda mrefu kwa
mahakama hiyo kuanza kusikiliza kesi za jinai kwani bado nchi nyingi za
Kiafrika hazijaidhinisha mkataba wa Malabo uliotolewa tangu Juni mwaka
jana ili kuanzisha hatua za usikilizwaji
wa kesi za jinai.
“Mpaka sasa
hakuna nchi hata moja iliyoidhinisha mkataba wa Malabo ambao ulitolewa tangu
juni mwaka jana hivyo itachukua muda mrefu mpaka mahakama iweze kusikiliza kesi
za jinai” Alisema Jaji Ramadhani
Ziara ya Raisi Kikwete kutembelea
Mahakama hiyo imetajwa kuwa ziara ya Mwisho ya Raisi huyo katika kipindi cha
Uongozi wake unaolekea tamati lakini pia
ni ziara ya kwanza ya Rais huyo tangu kuanzishwa kwa Mahakama ya Afrika.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia