Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akifafanua
jambo mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Tanga waliojitokeza kwenye
mkutano wa hadhara wa kampeni,uliofanyika katika viwanja vya Tangamano
jioni ya leo mjini Tanga.
Mgombea wa Urais
kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa mji wa Tanga
kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya angamano,jioni ya
leo ambapo aliahidi kuboresha Bandari ya Tanga, kujenga Viwanda vya matunda
na samaki ili kuweza kupunguza tatizo kubwa la ajira kwa
vijana.
Naibu Waziri wa Sheria na Katiba,ambaye pia ni mgombea
Ubunge viti maalum upande wa akina Mama mkoa wa Tanga (UWT),Mh Ummy Mwalimu
akimuombea Kura za kutosha mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli ili aweze
kuibuka mshindi na kuiongoza Tanzania katika awamu ya
tano.
Wakazi wa mji wa Tanga waliofika kwenye mkutano huo
wakishangilia jambo.
Nyomi la watu .
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akisalimiana
na Naibu Waziri wa Fedha na mgombea ubunge wa
Jimbo la Iramba Magharibi Mheshimiwa Mwigulu
Nchemba
Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ambaye pia ni mgombea
Ubunge wa Jimbo la Bumbuli Mhe. January Makamba akihutubia wakazi wa mji wa
Tanga kwenye mkutano wa kampeni za CCM.
Sehemu ya umati wa wakazi wa mji wa Tanga na vitongoji
vyake wakiwa wamefurika kwenye viwanja vya Tangamano kwenye mkutano wa
kampeni za CCM,ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli aliwahutubia
wananchi hao.
Dkt
Magufuli akisisitiza jambo mbele ya maelfu ya wananchi (hawapo pichani)
jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika uwanja wa
Tangamano.
Naibu
Waziri wa Fedha na mgombea ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi
Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akihutubia wakazi wa Tanga mjini kwenye mkutano
uliofanyika kwenye uwanja wa Tangamano.
Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ambaye pia ni mgombea
Ubunge wa Jimbo la Bumbuli Mhe. January Makamba na Naibu Waziri wa Fedha na mgombea ubunge wa
Jimbo la Iramba Magharibi Mheshimiwa Mwigulu Nchemba wakifuatilia
yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa kampeni jioni ya leo katika uwanja wa
Tangamano,ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alihutubia na Kumwaga
sera zake kwa wananchi,ikiweno na kuomba ridhaa ya kuwaongoza katika miaka
mitano ijayo.
Katibu Mkuu
Mstaafu wa CCM Mzee Yusuph Makamba akihutubia wakazi wa Tanga mjini kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika ndani ya viwanja vya
Tangamano.
Maelfu ya Wananchi wakimsikiliza Dkt Magufuli alipokuwa
akimwaga sera zake na kuwaomba wananchi hao wajitokeze kwa wingi Oktoba 25
na kumpigia kura ya ndio ili aibuke mshindi na kupewa ridhaa ya kuiongoza
Tanzania katika awamu ya tano.
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwaaga
wananchi wa mji wa Tanga waliofika kwenye mkutano hadhara wa
kampeni,uliofanyika jioni ya leo katika viwanja vya Tangamano mjini humo na
kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu.
PICHA NA MICHUZI JR-TANGA
PICHA NA MICHUZI JR-TANGA