Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi
Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia maelfu ya wananchi waliofurika
kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais,uliofanyika katika uwanja
wa Kawawa,mkoani Kigoma jioni ya leo. PICHA NA MICHUZI
JR-KIGOMA.
Dkt Mafuli amewaabia wananchi wa Kigoma
kwenye mkutano wa kampeni leo jioni kwenye uwanja wa kawawa kuwa Serikali
yake kwa sehemu kubwa itakuwa upande wa wananchi wanyonge ili
hatimaye wawe na maisha yenye neema,amesema kuwa Serikali yake haitakuwa ya
kunyanyasa mama
ntile na kudaiwa kodi za hovyo hovyo,amesema kuwa ataimarisha ukusanyaji wa
kodi kwenye serikali
yake, lakini pia atawabana wafayabiashara wakubwa ambapo baadhi yao
hawalipi kodi
Magufuli amewataka Wananchi kumuamini
kwa yale ambayo amekuwa akiyasema kwenye mikutano yake ya kampeni na
kuongeza anachoahidi ndicho ambacho atakitekeleza kwenye serikali yake
na kwenye maisha yake huwa hataki kutoa ahadi za
uongo.
Maelfu ya wananchi waliofurika kwenye
mkutano wa hadhara wa kampeni za
Urais,uliofanyika katika uwanja wa Kawawa,mkoani Kigoma jioni ya leo
wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa
akiwahutubia.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli
akiwahutubia maelfu ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa hadhara
wa kampeni za Urais,uliofanyika katika uwanja wa Kawawa,mkoani Kigoma jioni
ya leo.
Aidha hadi jana, tarehe 16 September 2015,
Mgombea Urais wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, alikuwa amekwishafanya
kampeni katika mikoa 12 na Majimbo 94. Amekwishafanya mikutano mikubwa ya
hadhara 76 na mikutano ya barabarani 381. Amekwishatembea, kwa gari, jumla
ya kilomita 13,720. Kwa ujumla amekwishakutana, moja kwa moja, na asilimia
zaidi ya 30 ya wapiga kura.
Wananchi na Mabango
yao
Mgombea
Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Nguruka
kwenye mkutano wa kampeni wa hadhara mapema leo
mchana.
Wakazi wa Nguruka waifuatilia
Mkutano.
Mgombea
Urais wa CCM Dkt Magufuli akimkabidhi Ilani ya chama cha CCM kwa
Mgombea Ubunge wa Kigoma Kusini,Hasna Mwilima na pia kummwombea kura kwa
wananchi mapema leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika
Nguruka mkoani Kigoma.
Wananchi wakisikiliza sera za Mgombea Urais
wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
Baadhi
ya Wananchi wa Uvinza wakiwa wamefunga barabara wakitaka wasikilizwe
kero zao na Mgombea Urais wa CCM,Dkt Magufuli alipokuwa akipita mjni
humo akielekea Kigoma mjini kwenye mkutano wa
hadhara.
Baadhi ya akina mama wakishangilia
jambo
Mgombea
Ubunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini Peter Selukamba akiwahutubia
wananchi wa Kalinzi,mkoani Kigoma kweny mkutano wa kampeni za Uraisi
jioni ya leo.
Baadhi
ya wafuasi wa chama cha CCM wakifuatilia mkutano wa hadhara katika
kijiji cha Kalinzi,ambapo mgombea Urais wa CCM Dkt Magufulia
aliwahutubia wananchi.
Wakazi wa mji wa Nguruka,mkoani Kigoma
wakifuatilia mkutano wa hadhara
Wananchi na mabango
yao
Kada
maarufu na aliyewahi kuwa Katibu MKuu wa CCM,Mh Yusuph Makamba
akisalimiana na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia
chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli kabla ya kupanda jukwaani na
kuwaomba ridhaa wakazi wa kigoma ya kuwaongoza katika awamu ya
tano.
Wananchi wakishangilia jambo kweye mkutano
wa kampeni za Urais
Wananchi wakifuatilia mkutano wa
kampeni
Kada
maarufu na aliyewahi kuwa Katibu MKuu wa CCM,Mh Yusuph Makamba
akiwahutubia wananchi wa Kigoma na vitongoji vyake jioni ya leo kwenye
mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais,uliofanyka katika uwanja wa
Kawawa mkoani Kigoma