Na Woinde Shizza,Arusha
TIMU ya
panone FC ya mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro maarufu kama matajiri wa
mafuta ,inatarajia kuanza kutupa karata yake ya mchezo wa kwanza wa ligi
daraja la kwanza(FDL) dhidi ya maafande wa JKT Oljoro ya jijini Arusha.
Mchezo huo utafanyika septemba 19 mwaka huu, katika uwanja wa Ushirika mjini moshi mkoani kilimanjaro,ambapo baada ya mchezo huo pia wataikaribisha timu ya Polisi Tabora semptemba 26.
Katibu wa timu ya Panone FC Augstino mwakatumbula alisema kuwa msimu huu wanaenda kuanza ligi daraja la kwanza ambapo kila mchezo kwao ni fainali na watahakikisha wanatinga kucheza ligi kuu msimu wa 2016-2017.
“Tulifanya usajili mzuri wa wachezaji 7 ambao wameungana na wachezaji wetu tuliokuwa nao msimu uliopita na tunaimani
wataisaidia timu hii na tuna jumla ya wachezaji 27 wanaounda kikosi cha
timu pia hatukuweza kuwasajili wote waliokuwepo hapo mwanzo na ni kutokana na matatizo mbalimbali yakiwemo wengine kutokuwa na nidhamu,uwezo wao umeshuka kimchezo.”alisema Mwakatumbula .
Aliwataja wachezaji hao saba ambao wamefanikiwa kusajiliwa na matajiri hao wa mafuta kuwa ni pamoja na Ally Mseja ambaye ni mchezaji huru na Abdallah Shauri ‘Machopa’ aliyetokea timu ya Lipuli –Iringa wote wakiwa ni washambuliaji, Florence Haure kutoka academy ya Kitayosce ya mkoani Kilimanjaro, Frank Kijoti aliyetokea AFC Arusha Rashid Gumbo kutoka Kinondoni Manispaa ambaao wote ni Kiungo,Maulid Khalid kutoka Singida United ambaye ni winga,Mansoul Mansoul kutoka Coastal Union ya Tanga ambaye ni golikipa.
Timu
hiyo ya Panone FC ipo kambini miezi miwili sasa ikijiweka tayari kwa
ajili ya michuano hiyo ya ligi Daraja la kwanza ambapo inatarajiwa
kucheza michezo ya kirafiki mapema wiki hii na timu za African sports,Magambo JKT na Coastal Union zote za Tanga .
Matajiri hao wa mafuta wananolewa na kocha Atuga Manyundo akisaidiwa na msaidizi wake Azizi Nyoni .
Ligi
daraja la kwanza ina shirikisha jumla ya timu 24 zilizogawanywa katika
makundi matatu ambapo timu ya Panone ipo katika kundi ‘C’ na timu za JKT
Olojro- Arusha,Polisi Mara –Mara,Rhino Rangers –Tabora,Mbao fc
–Mwanza,Polisi Tabora -Tabora,Geita Gold –
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia