DC AMCHAPA KIBAO MWANANAFUNZI KISA CHATA YA CHADEMA

MKUU wa wilaya ya Mbulu mkoani Manyara,Anatory Choya amekanusha vikali kauli iliyotolewa na mmoja kati ya washiriki wa mdahalo wa wagombea ubunge jimboni humo kuwa aliwachapa viboko wanafunzi wa shule moja ya sekondari baada ya kuonyeshwa alama ya V.



Katika mdahalo huo uliofanyika juzi mjini Mbulu,mmoja kati ya washiriki hao Michael Tluway aliuliza swali kuwa hatua gani atachukuliwa mkuu huyo wa wilaya baada ya kuwachapa wanafunzi wa shule ya sekondari waliomuonyesha ishara ya V na yeye kuwaonyesha alama ya dole gumba.



Akijibu swali hilo mgombea ubunge jimboni humo kwa tiketi ya Chadema Mustapha Akoonay alisema mkuu huyo wa wilaya anapaswa aende likizo hadi uchaguzi ufanyike kwani amekuwa akiibeba CCM.



Mdahalo huo ulioandaliwa na Asasi za kiraia mkoani Manyara (MACSNET) kwa ushirikiano na The Foundation for Civil Society ulihusisha wagombea wa vyama vya CCM,CUF na Chadema lakini ulihudhuriwa na Mustapha Akoonay peke yake mgombea wa chadema.



Akifafanua kuhusu hilo mkuu huyo wa wilaya ya Mbulu alisema yeye hakuwaonyesha wanafunzi hao alama ya dole gumba inayotumiwa n a CCM bali alikuwa anapita kwenye eneo la shule hiyo iliyopo kata ya Tlawi na ndipo wanafunzi hao wakamzomea.



“Watoto hao walikuwa wakinionyesha ishara ya vidole viwili inayotumiwa na wapinzani huku wakinizomea hivyo kama mzazi ilinibidi niwabane na kuwauliza kwa nini wananifanyia hivyo,” alisema.



Alisema kuwa baadhi ya watoto hao walimweleza kuwa wameagizwa na mmoja kati ya wagombea ubunge kuwa wawazomee viongozi wa CCM na Serikali kila mahali watakapowakuta na pia wawaonyeshe ishara ya V.



Choya alisema mmoja kati ya wanafunzi hao aliyetambulika kwa jina moja la Paschal aliomba msamaha kwa niaba ya wanafunzi wenzake na pia alikiri kwa maandishi kuwa hawatarudia tena kosa hilo .



Alisema maneno yaliyozungumzwa kuwa aliwachapa wanafunzi hao ni yakupikwa na watu wasio makini na kuongeza kuwa wanatakiwa wazungumze sera ya vyama vyao siyo kuzusha uongo.



“Mimi ni kiongozi wa Serikali siyo wa chama nahakikisha majukumu yangu kama mlinzi wa amani wa wilaya yanazingatiwa hivyo siwezi kuwa na hofu yeyote ya kuhakikisha amani inakuwepo,” alisema Choya.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

إرسال تعليق

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia