Zaidi ya watendaji na wenyeviti kutoka halmashauri za wilaya 5 zinazotekeleza
mradi wa Ufugaji wa asili unaoendeshwa na jumuiko la Maliasili
Tanzania(TNRF)wameshiriki katika mafunzo ya siku 5 juu ya mfumo wa
ufugaji asili, uchambuzi wa Sera na utetezi katika maeneo yao.
Semina
hiyo iliyofunguliwa na kufungwa na makamu mwenyekiti wa halmashauri ya
mji wa Babati John Teu alisema kuwa famila nyingi hapa nchini na za
jamii ya kifugaji hutegemea mifugo kwa chakula na kipato na kuwa ni
aghalabu sana kumkuta mfugaji akijishirikisha na kilimo.
Teu
alisema kuwa ipo haja kwa wafugaji wa kiasili kuanza kudai haki ya
umiliki wa njia za kuipatia mifugo malisho ya kiasili kama wafanyavyo
mataifa yalioendelea na huu utakuwa ni utamaduni wa kuhama hama ambao
hata unaweza kuingizwa kwenye mfumo wa sera za nchi yetu.
Aidha
makamu mwenyekiti huyo alisema kuwa sera za mfugaji wa asili ambaye
kiuhalali ni muhamaji kutoka eneo mmoja kwenda jingine kote duniani
inafaa kuweka wazi na kuwatengea maeneo ya mizunguko yao
wakati wakifuta malisho huku akutolea mfano wa taifa la Hispania ambalo
wafugaji wanahama kila msimu.
“Tunatakiwa
kuiga taifa hilo kwani wafugaji wamekuwa wakihama hama na kuleta picha
nzuri wakipita katikati ya mitaa kuelekea kwenye eneo wanalohamia na
watalii wengi hufuata utalii huu na serekali hupata faida mara
mbili”alisema Teu
Nae
mratibu wa Semina hiyo Zakaria Faustin alisema kuwa mafunzo hayo ya
siku tano yalienda sambamba na kujifunza juu ya mfumo wa ufugaji wa
asili,utungaji sera na utetezi kwa wafugaji wa asili na kuwa
yamewashirikiasha wenyeviti kutoka wilaya 5 zinazotekeleza mradi wa
taasisi hiyo huku akiwataja wataalamu wenzake waliondesha nae mafunzo hayo kuwa Alais Morindat na Emanuel Sitayo huku akisema kuwa semina hiyo imewashirikisha zaidi ya wanasemina 40.
Alisema kuwa mafunzo hayo ni muundelezo wa kutekeleza miradi iliyotolewa ruzuku kwa asasi zaidi ya 18 zinazotekeleza kusaidia uelewa
kwa wafugaji wa asili kama imetoa matunda hivyo sasa wanawapa mafunzo
kama hayo kuweza kuweka changamoto katika kukabiliana na changamoto za
ufugaji wa asili hapa nchini.
Alisema
kuwa miongoni mwa wataalamu na viongozi wa halmashauri za wilaya zilizo
shiriki ni pamoja na Longido,Babati,Kilindi,Kahama,Kilosa na Gairo na
wataalamu kutoka wizara ya Ardhi huku akitegemea kuwa mafunzo waliopata
wataenda kutetea haki na kuulinda ufugaji wa asili kwenye maeneo yao.