CHEKI BANDA LA RADIO 5 UNAKARIBISHWA KUTEMBELEA PINDI UFIKAPO KATIKA VIWANJA VYA TASO NANE NANE UWAONE WATANGAZAJI KIBAO LIVE
Kampuni ya Tan Communication
Media inayo miliki kituo cha Radio 5 chenye makao yake makuu jijini
Arusha imetangaza punguzo la asilimia 30% kwa matangazo kwanzia tarehe 1
hadi 10 mwezi huu katika sherehe za nane nane zinazoendelea hapa Nchini
Akitangaza punguzo hilo Meneja
masoko wa kampuni hiyo Sarah Keiya amesema kuwa ofa hiyo ni maalum kwa
kipindi hichi cha sherehe za nane nane huku akiwataka wafanyabiashara
wote wakubwa na wadogo kuchangamkia fursa hiyo
“Tumepunguza bei yetu ya matangazo kwa asilimia 30% hivyo ni fursa nzuri kwa wafanyabiasha kutangza biashara zao “alisema Keiya
Aidha alisema kuwa kwa sasa
kituo cha Radio 5 kimeongeza masafa na inasikika katika mikoa 18 ya
Tanzania hivyo husikika hata nje ya nchi ambapo Mombasa Kenya inasikika
kupitia masafa ya Tanga 98.9 na Dar es saalam inasikika kupitia masafa
ya 91.3
“Hizi ni habari za kuwanufaisha wafanyabiashara pamoja na wasikilizaji wetu kutokana na sisi kuongeza masafa zaidi”alisema Keiya
Hata hivto aliongeza kuwa siku
ya jumatatu ya tarehe 5 kutakuwepo na mashindano mbalimbali ya michezo
itakayokuwa ikisimamiwa na kituo cha radio 5 katika banda lao lililopo
katika viwanja vya nane nane njiro ambapo itawashirikisha wafanyakazi wa
kituo hicho,wanafunzi na wapenzi wa kituo hicho
Alisema kuwa zawadi
zimeshaandaliwa kwaajili ya washindi huku akitaja zawadi hizo kuwa ni
simu za mkononi,mipira,kofia na ofa ya kurekodiwa nyimbo bure
Michezo itakayokuwa ikirindima siku hiyo ni pamoja na kuimba,kula na kunywa,kucheza, na nk
“Nawashukuru sana wadhamini wetu ambao ni Killiative printer,Arusha record,Pepsi”alisema Keiya
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia