CHEKI BANDA LA RADIO 5 UNAKARIBISHWA KUTEMBELEA PINDI UFIKAPO KATIKA VIWANJA VYA TASO NANE NANE UWAONE WATANGAZAJI KIBAO LIVE

DSCF0035Taswira katika banda la Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha katika viwanja vya nane nane njiro
DSCF0042Wafanyakazi wa kituo cha Redio 5 wakiwa katika banda lao katika viwanja vya nane nane njiro Arusha
DSCF0039Katikati ni meneja masoko wa kampuni ya Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 Sarah Keiya,kushoto ni Clara moita na Ashura Mohamed watangazaji maarufu wa kituo hicho wakiwa kwenye banda lao katika viwanja vya nane nane njiro Arusha
DSCF0034Hapa ni Production meneger Deo Gee maarufu kama “dj Deo G” na Tonnie Kaisoi wakiweka mambo  ya muziki sawa
DSCF0049Meneja masoko wa Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio5 Sarah Keiya na Pamela Mollel mmiliki wa http://jamiiblog.co.tz katika pozi 
DSCF0050Ashura Mohamed mtangazaji na mwandishi wa Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha akiwa katika pozi na Meneja masoko wa kampuni hiyo Sarah Keiya
DSCF0044Dj Deo G na Sarah Keiya wakiwa wanafurahia jambo ndani ya banda la Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5
Kampuni ya Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha imetangaza punguzo la asilimia 30%  kwa matangazo kwanzia tarehe 1 hadi 10 mwezi huu katika sherehe za nane nane zinazoendelea hapa Nchini
Akitangaza punguzo hilo Meneja masoko wa kampuni hiyo Sarah Keiya amesema kuwa ofa hiyo ni maalum kwa kipindi hichi cha sherehe za nane nane huku akiwataka wafanyabiashara wote wakubwa na wadogo kuchangamkia fursa hiyo
“Tumepunguza bei yetu ya matangazo kwa asilimia 30% hivyo ni fursa nzuri kwa wafanyabiasha kutangza biashara zao “alisema Keiya
Aidha alisema kuwa kwa sasa kituo cha Radio 5 kimeongeza masafa na inasikika katika mikoa 18 ya Tanzania hivyo husikika hata nje ya nchi ambapo Mombasa Kenya inasikika kupitia masafa ya Tanga 98.9  na Dar es saalam inasikika kupitia masafa ya 91.3
“Hizi ni habari za kuwanufaisha wafanyabiashara pamoja na wasikilizaji wetu kutokana na sisi kuongeza masafa zaidi”alisema Keiya
Hata hivto aliongeza kuwa siku ya jumatatu ya tarehe 5 kutakuwepo na mashindano mbalimbali ya michezo itakayokuwa ikisimamiwa na kituo cha radio 5 katika banda lao lililopo katika viwanja vya nane nane njiro ambapo itawashirikisha wafanyakazi wa kituo hicho,wanafunzi na wapenzi wa kituo hicho
Alisema kuwa zawadi zimeshaandaliwa kwaajili ya washindi  huku akitaja zawadi hizo kuwa ni simu za mkononi,mipira,kofia na ofa ya kurekodiwa nyimbo bure
Michezo  itakayokuwa ikirindima siku hiyo ni pamoja na kuimba,kula na kunywa,kucheza, na nk
“Nawashukuru sana wadhamini wetu ambao ni Killiative printer,Arusha record,Pepsi”alisema Keiya

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia